Google PlusRSS FeedEmail

WAKATI WASANII WAKIONESHA ITIKADI ZAO ZA VYAMA, HAYA NI MANENO YA RAY



Joto la uchaguzi linaendelea kuongezeka kila kukicha kuelekea Oktoba, vyama mbali mbali vinaendelea kujinadi kwa sera na mipango yao.

Wasanii kadhaa wa muziki na maigizo tayari wameanza kuonesha mlengo wao, na mapenzi yao kwa vyama mbalimbali.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, Bazil Jonas amedai haifai kwa wasanii ambao ni kioo cha jamii kujigawa kimakundi, kwa kuwa itikadi na kazi zao ni vitu viwili tofauti.

PRO24DJs imezinyaka post mbili za msanii Vicent Kigosi ‘Ray’ na mbunifu wa mavazi Martin Kadinda, ambazo zina tija kwa vijana kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu.

“Siasa siasa siasa siasa: Now nashukuru Kwa kunipa sababu ya kuweza kufanya maamuzi ninayotegemea kufanya… Ila kwanza ningeanza kwa kuuliza swali ni wapi uliona demokrasia inahitaji vurugu?? Wapi uliona mabadiliko yanaletwa kwa kejeli, dharau na Fujo?? Wapi nchi watu wanataka wakitakacho bila kuwa na sababu za kueleweka… Najikuta nahama chama na imani niliyojijengea baada ya kuona wafuasi wenzangu wanafanya mambo yasiyopendeza kwa watu wenye ushabiki wa chama kingine… Swala la ufisadi, ulafi wa madaraka na tamaa za nyazifa ni swala la mtu binafsi au kiongozi husika… Lakini kumzomea mfuasi wa chama hicho ni swala na kumzomea mtoto kwakuwa babake ni mlevi… Baba kuwa mlevi haimaanishi na mtoto ni mlevi…. Nasubiri kusikia sera za wagombea ili niamue kura yangu nampa nani… Ila kwa hali ilivyo sasa sitegemei kuwa shabiki wa mwanasiasa anayechochea uvunjifu wa amani… Mwanasiasa anayetumia majukwaa kuchafua chama kingine… Weka sera zako mbele na tutakupa kura we ukikazana na kunyooshea vidole wagombea wengine utaishia kupigiwa kura na familia yako na walafi wenzako… Mimi kura yangu lazima niweke eneo salama pale penye kampeini za amani… Utulivu… Na kikubwa siasa ni burudani… Ukiona chama chako kinakutoa jasho la hasira na chuki hicho si chama… Jasho langu liwe ni faraja na nuru ya Tanzania yenye amani na utulizu… Umaskini wetu sote na tutaepukana nao kwa kutafuta maarifa ya kujiendeleza kimaisha…. Naipenda nchi yangu sanaaaaaaa #MUHIMU: UKIONA HUKUBALIANI NA NISEMALO WE PITA KIMYA UKITUKANA BLOCK ITAKUHUSU MAANA MMEZIDI KUTUPANGIA MAISHA” ameandika Martin.

“Usiku wa jana nimetafakari vi2 vingi sana kuhusu Nchi yangu iliyobarikiwa kila aina ya utajiri wa madini mbuga za wanyama wakiwemo aina mbalimbali za wanyama wa kuvutia na hekta kubwa za misitu Ila ninaona vipofu wengi sana wasiolewa nini 2lichobarikiwa ndani ya Tanzania ye2. 2meingizwa mikenge mingi sana katika mikataba tena mibovu bajeti kandamizi Kwa wa2 wa hali ya chini mifumuko ya bei kila kukicha hali ngumu kwa wasanii wa Tanzania kila siku ahadi zisizotekelekeza why nasema hivyo wasanii wenzangu? 2meumia kwa kipindi kirefu sana bila msaada wowote ha2na haki miliki wa kazi ze2, zinaibiwa kama njugu sokoni kariakoo yani 2li2pwa kama taka taka kwenye dampo lakini sasa hivi kipindi cha uchaguzi ndio 2naonekana umuhimu we2 tuamke kuwaambia wananchi wachague viongozi makini watakaoweza ku2vusha Watanzania kwenda ha2a nyingine.

Tuna wa2 wengi sana nyuma ye2 wanaotuamini sisi wasanii kama kioo cha jamii tusiwapoteze Watanzania kuwaambia Viongozi wa chama flani ndio wanafaa kwa vijisenti vidogo 2navyopewa. Watanzania huu ni wakati sahihi waku2lia na kuwachagua viongozi makini wanaofaa Ni katika kukumbushana 2 waswahili wanasemaje utakaokatanao kuni ndio utakaota nao moto.” ameandika Ray.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging