Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WAHAMASISHA KUCHAGUA MABADILIKO OKTOBA MWAKA HUU


 Msanii wa kizazi kipya nchini Ney wa Mitego akitumbuiza mshabiki waliojitokeza kwa wingi katika tamasha la wazi lililokuwa na lengo la kuhamasisha wasanii na wananchi kuchagua mabadiliko


 Mbunge aliyekwisha maliza muda wake wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya 'Sugu' akitumbuiza mashabiki wake jana katika tamasha la wazi lililofanyika katika uwanja wa  Mbagara Zakhem jijini Dar es Salaam, tamasha hilo lilipewa jina la 'Democracy in Dar'.




WASANII mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, washiriki tamasha la ‘Democracy in Dar’ lililofanyika Jumapili katika viwanja vya Zakhem Mbagala, lililokuwa na lengo la kuunganisha wasanii katika kukuza democracy na kuimiza wananachi kuchagua mabadiliko ifikapo Oktoba mwaka huu.

Ambapo jumuiko hilo lilijumuisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya, muziki wa Injili,waigizaji wa filamu, muziki wa asili na wachoraji wa katuni wote kwa pamoja walijumuika katika tamasha hilo la bure kuhamasisha vijana, na wananchi kwa ujumla sambamba na kuwapatia burudani nzuri.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ambaye pia ni msanii wa bongo fleva ‘Sugu’ alisema muunganiko huo wa wasanii wanaamini kuwa mabadiliko ya serikali yanaweza kusaidia kupata serikali itakayosikiliza na kushughurikia changamoto zao halisi.

“Hali ilivyo sasa wasanii walio wengi wanatumika kisiasa zaidi kwa mahitaji ya wanasiasa tofauti na wasanii wanachokitarajia, kupitia muunganiko huu ndio wakati wa sisi wasanii kuungana kwa pamoja kuchagua mabadiliko ili tuweza kupata serikali itakayoweza kutetea na kutatua changamoto za wasanii” alisema Sugu.

Aliongezea kuwa muunganiko huo hakuangalia itikadi za vyama vya kisiasa bali umelenga wasanii wote wenye mawazo sawa na lengo moja la kuchagua mabadiliko, ambapo walitumia nafasi hiyo na vipaji vyao kuhamasisha wananchi kuungana pamoja kuchagua mabadiliko kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Mbali na hilo aliongezea kuwa kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura anatakiwa kutunza shahada yake ili aweze kuwa na sifa za kupiga kura ifikapo Oktoba mwaka huu.

Tamasha lingine la aina hiyo litafanyika katika mikoa ya Tanzania bara na visiwani na wananchi ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuhamasisha na kuhimiza jamii kujitambua na kuchagua mabadiliko na kuacha kutumika kwa maslahi ya wachache.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging