Google PlusRSS FeedEmail

TI AMZUNGUMZIA YOUNG THUG

Young Thug ni rapa aliyefanikiwa kuteka soko la muziki kwa haraka zaidi mara tu alipofanikiwa kusikika masikioni mwa wadau wa muziki.

Style yake ya uandishi na mtindo wake wa kurap kama kuimba umefanya jamaa huyo kutoka Atlanta kupata features nyingi toka kwa mastaa mbalimbali wa muziki.

Lakini pamoja na utamu wake wa kazi ya muziki, maisha yake yamekuwa yakiwashangaza jamii kutoka na life style yake ya kustafsiriwa kama ni mkorofi.

Sasa rapa TI ameibuka na kuitaka jamii kuacha kutafsiri vibaya juu ya maisha ya rapa huyo kwani kila mtu ana haki ya kuishi vile anavyotaka.

TI amewataka wadau kuendelea kazi ya msanii huyo na sio kufuatilia maisha yake nje ya muziki.

‘Inabidi watu waangalie kazi yake zaidi na sio maisha yake nje ya muziki, Thug ni msanii mkali anayeweza kwenda na soko la muziki was as” alisema TI.

Pia TI ameweka wazi kwamba kwenye albamu yake mpya inayofuata sauti ya Thug itasikika kwenye moja kati ya ngoma zilizopo kwenye albamu hiyo.

TI amesema Thug anauwezo mkubwa ndio maana ameamua kumshirikisha tena kwa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kufanya poa kwenye ngoma ya All About Money.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging