Google PlusRSS FeedEmail

TREVOR NOAH KUMRITHI JON STEWART KWENYE THE DAILY SHOW

                                        Msanii kutoka Afrika Kusini Trevor Noah alifungua ukurasa mpya usiku wa kuamkia leo alipoandaa shoo yake ya kwanza ya ''The Daily Show'' na kuchukua pahala pake muigizaji nguli, Jon Stewart .

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliteuliwa kuandaa maonyesho ya kipindi hicho maarufu cha kuchekesha kwenye runinga ya Comedy Central.Kwa mujibu wa tovuti inayotathmini maswala ya usanii 'Variety' raia huyo wa Afrika kusini hakuwa na msisimko.

Deadline kwa upande wake iliandika kuwa hakuwa na cheche zozote katika shoo yake ya kwanza.Mchambuzi wa vipindi vya runinga Brian Lowry amesema kuwa onyesho hilo lilimpa sura mpya ya kuwa mkakamavu zaidi ya hapo awali alipokuwa akitumika kama mchekeshaji aliyeigiza kama ripota.

Stewart alijiuzulu baada ya kuandaa kipindi hicho cha ''The Daily Show'' kwa miaka 16.Kwa upande wake Noah aliteuliwa kumrithi mwezi machi.Marejeo ya kipindi hicho itakuwa leo usiku kwenye runinga ya Comedy Central at saa saba usiku wa leo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging