Google PlusRSS FeedEmail

IZZO BUSINESS ATOA CHANGAMOTO KWA RAIS AJAYE

Star wa Hip Hop Bongo Izzo Business, ametoa mtazamo wake na sifa za Rais atakayekwenda kumchagua Octoba 25 mwaka huu.

Akizungumza kupitia kipindi cha The Jump Off  Izzo amesema Rais ajaye anatakiwa awe muelewa wa kuangalia nyanja za ujambazi zilizoongezeka, jinsi atakavyofufua viwanda vilivyo kufa.

“Mimi napenda kwanza nimtambue kama baba, maana sisi ndio tunakuwa kama watoto kwake, aweze kutuongoza wanae kuyafikia maendeleo zaidi, atatue tatizo la Ajira, Aongeze kasi ya kiuchumi na kuangalia sekta ya viwanda.

“Unajua sasa hivi ukiangalia ujambazi umeongezeka kwa sababu vijana hawana ajira, kwa hiyo awe tu baba mwenye uelewa wa mambo mengi” Alisema Izzo.

Katika ‘line’ nyingine, mkali huyo kutoka Mbeya alifafanua kwanini hashiriki katika kampeni kwenye uchaguzi wa mwaka huu, amedai anaogopa kuwagawa mashabiki wake katika makundi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging