WASANII WA FILAMU KUTAFUTIWA SOKO NJE
Wasanii wa filamu nchini Tanzania wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao nchini London Uingereza na kampuni ya Mad Mad iliyopo nchini humo kwa lengo la kukuza sanaa hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Yasmin Razak alisema kuwa ameamua kufanya kazi na wasanii wa hapa nyumbani ili kuwakwamua kiuchumi pamoja kukuza tasnia ya filamu
Alisema kuwa kwa muda mrefu amekaa London lakini hajaona maendeleo yoyote ya tasnia hiyo hivyo akafikiria kitu cha kufanya ili kuisaidia tasnia hiyo ya filamu, kwa kila mkataba wake msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha shilingi milioni 50 pamoja na malipo mengine yaliyopo kwenye mkataba huo
"Licha ya kupata kiasi hiko pia msanii ataweza kupata asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nyumbani" alisema Razak