TYSON AELEZEA SABABU ZINAZOICHAFUA TASNIA YA FILAMU
Kutokana na kashfa ya rushwa ya ngono kuikumba tasnia ya filamu Tanzania mtayarishaji wa filamu nchini Geoge Tyson aelezea chanzo cha rushwa hiyo ni kutokana na ukosefu wa elimu kwa baadhi ya waandaaji wa filamu nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam Tyson alisema kuwa rushwa inachangiwa na waandaaji wa filamu kukosa maadili ya kazi na hali ambayo imesababishwa na kukosa elimu ya uaandaaji wa kazi hiyo na matokeo yake kuchukua watu wasio na sifa na kipaji cha uigizaji
Tyson aliweka wazi kuwa wengi wa waandaaji hao wamepata uzoefu wa kile wanachokifanya kupitia kazi walizokuwa wakifanya hali inayochangia unyanyasaji kwa watu wengine wenye sifa ya kuwa waigizaji na ndio maana katika tasnia hiyo imejaa wababaishaji na siyo wenye vipaji
"Ukiwa msichana mrembo na mwepesi kutongozeka ni rahisi kupata nafasi ya kuigiza ila ukiwa mgumu na wa kawaida hata kama unakipaji siyo rahisi kupata nafasi ya kuigiza kitu ambacho si kizuri kwa ajili ya kukuza fani ya uigizaji" alisema Tyson
Pamoja na hayo aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya waandaaji wanatumia kambi kama njia ya kurahisisha kukutana kingono na baadhi ya washiriki wa filamu, wakati hapo mwanzo hakukuwa na maswala ya kambi na hakuna umuhimu wa kuwa na kambi
Tyson alielezea jinsi kambi zilivyokuwa hazina umuhimu kwenye tasnia ya filamu na kutoa mfano kuwa watu wenye umuhimu wa kuwa na kambi ni wacheza mpira