WASANII WA SARAKASI WAFUNDWA
Kutokana na kuwa na ukosefu wa ajira wasanii wa mchezo wa sarakasi washauriwa kuupa kipaumbele mchezo huo ili waweze kujiajiri kupitia sana hiyo
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam jana na aliyekuwa Ofisa Sanaa mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Omary Mayanga katika jukwaa la sanaa
Alisema kuwa vijana wanatakiwa watafute fursa mbalimbali kwa ajili ya kupata mafunzo ya sarakasi kwani chuo kilichokuwa kinatoa mafunzo hayo kwa sasa hakina nafasi baada ya kukosa nafasi hiyo kwa sababu wanatoa mafunzo kwa Maofisa Utamaduni
Alisema kuwa vijana watumie fursa ya kujiendeleza kutumia mchezo huyo kama sehemu moja wapo ya kupata ajira na kujiongezea kipato ili waweze kutengeneza maisha yao ya kila siku
Mayanga alitumia pia nafasi hiyo ya kuwatoa hofu vijana wanaotaka kujiunga na mchezo wa sarakasi huku akisisitiza kuiondoa dhana ambayo wameijenga kichwani mwao kuwa mchezo huo unasababisha ugumba