Nyota wa muziki wa kizazi kipya na balozi wa kampeni ya kuzuia malaria nchini, Elias Barnaba amesema kuwa atayatumia mafunzo ya kupambana na Malaria atakayoyapata nchini Afrika Kusini, kuwaelemisha watanzania hasa wa vijijini mbinu za kupambana na ugonjwa huo.
Msanii huyo na mabalozi wenzake wa Malaria, Amini Mwinyimkuu na Linah wanatarajia kuondoka nchini mwezi huu kuelekea Afrika Kusini kuhudhuria mafunzo hayo yatakayochukua muda wa mwezi mmoja.
Barnaba alisema kuwa yeye binafsi ameshawahi kupoteza ndugu yake wa karibu kutokana na ugonjwa huo, hivyo hataki kuona watanzania wanaendelea kuteketea kwa ugonjwa huo unaoongoza kwa kuua watu wengi duniani.
‘Nimewahi kupoteza ndugu yangu wa karibu sana kutokana na ugonjwa huu, inaniuma sana kwa kweli. Nitakaporudi, nitafanya kila njia kuhakikisha watu wanapata elimu hii,” alisema msanii huyo.