Google PlusRSS FeedEmail

DIAMOND PLATNUMZ AKIWA NA MTOTO WAKE

[Read More]

                                          Bicco Mathew

WAKATI msemo wa Hapa kazi ukiwa ndio habari ya mjini na sisi tunasema “ FILAMU KAZI” jukwaa la Wanaharakati wa maendeleo ya filamu Tanzania limeundwa na linaendelea kufanya vema kuelekea kutafuta suruhu au dawa ya soko la filamu kwa kuangazia matatizo au changamoto zinazo ikabili tasnia hiyo yenye uwezo wa kuajiri watu wengi pengine kuliko sekta yoyote

Katibu wa JWMFT Bicco Mathew amsema kuwa wadau walikutana katika Hoteli ya Valentino iliyopo Kariakoo kuitikia wito wa Ndg. Myovela Mfwaisa juu ya kuhudhuria kwenye mjadala wa juu ya namna gani tutaisaidia tasnia ya Filamu nchini kupata soko nje ya mipaka ya Tanzania, kuleta hamasa kubwa kwa wadau waliohudhuria katika kikao hicho huku kila mdau akichangia kwa umakini zaidi.

“Hapa mimi naongea kama mwanaharakati pia nitafafanua baadhi ya mambo ambayo inaoneka kama TAFF imeshindwa kufanya lakini ukweli ni kwamba siku zote tunapigania kupata sera ya filamu,”

“Ni kweli kimaandishi Serikali imerasimisha filamu lakini Wizara husika imeshindwa kuonyesha dira ili tasnia ya filamu iweze kupata sera ambayo ndio kitu muhimu sana kwa sasa,”alisema Bicco.

Wajumbe John Kallaghe, Gallus Mpepo walishauri kuwa kuna haja ya wasanii kuhudhuria semina pamoja shule za muda mfupi ili kukabilia na ushindani wa filamu za kimataifa kama legho likiwa kufika katika soko la kimataifa.

Aidha mwigizaji wa siku nyingi Bakary Masasi alisema kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinadumaza wasanii kwa kuwakatisha tama kuwa baada ya kifo cha marehemu Steven Kanumba filamu imeshuka kitu ambacho anasema si kweli bali ubunifu umepotea.

MAENDELEO YA FILAMU TANZANIA

                                           WAKATI msemo wa Hapa kazi ukiwa ndio habari ya mjini na sisi tunasema “ FILAMU KAZI” jukwaa ... [Read More]

ALBAMU YA ADELE KUWEKA HISTORIA MPYA UK

                                 Albamu ya mwanamuziki Adele huenda ikaweka historia nchini Uingereza kwa kuwa albamu iliouza zaidi ,ikiwa ... [Read More]

Kuna habari njema,mtandao wa facebook umetangaza kuwa unatafuta mbinu mpya ya kupunguza machungu unayopata wakati unapokutana na mpenzi wa zamani ambaye muliwachana baada ya ugomvi.

Kwa sasa,iwapo hutaki kukumbushwa kuhusu mpenzi huyo wa zamani una uwezo wa kumuondoa kama rafiki ama hata kumzuia asiweze kukuona katika mtandao wa facebook.

Tatizo ni kwamba watajua kwamba umechukua hatua kama hiyo ambayo sio nzuri sana.

Mahusiano katika mtandao wa facebook ni swala muhimu sana,kama alivyosema jaji mmoja kutoka mjini New York, kwamba unaweza kutuma wito wa talaka katika mtandao huo na uwe halali.

Lakini kifaa kipya cha mtandao wa facebook kinalenga kubadilisha kile ambacho mpenzi wako wa zamani anaweza kuona,bila kujua kwamba kuna kitu umefanya..

Kipengele hicho kinaruhusu:

*Kutoliona mara kwa mara jina la mpenzi wa zamani pamoja na picha yake bila kuiondoa ama kumzuia kukuona.

*Weka usimamizi wa ni nani anayeweza kuona picha zako na mpezi wako wa zamani na uziondoe katika machapisho yenu pamoja.

*Wakati facebook ilipozinduliwa katika taasisi na vyuo vikuu,lengo lake lilikuwa machapisho ya mahusiano.Ni hatua ya kidijitali ambayo ilisaidia mda wa wengi.


Lakini hivi majuzi,watu wamekuwa wakichukua tahadhari wanapotangaza uhusiano wao katika facebook.

Watu walikuwa wakitumia neno ”its complicated” kwa uhusiano ambao unaelekea kugonga mwamba na badala yake watu wanatumia maneno ya kidunia kama vile ‘kuchumbiwa’ ama hata ‘kupata mtoto’.

Hatahivyo kifaa hicho kipya kitaanza kutumika hivi karibuni,imesema facebook.


Mpango huo ni mongoni mwa juhudi zinazoendelea kuendeleza raslimali za watu wanaokabiliwa na wakati mgumu katika maisha yao,aliandika Kelly Winters meneja msimamizi wa bidhaa za facebook.

”Tunaamini kifaa hicho kitawasaidia watu kumaliza uhusiano wao katika facebook kwa urahisi na udhibiti.Iwapo unatumia simu ya mkononi nchini Marekani unaweza kukitumia kifaa hicho mara moja kwa kuvunja uhusiano na mpenzi wako”.

FACEBOOK KUANDAA UTARATIBU WA KUTOONA TAARIFA ZA X WAKO

Kuna habari njema,mtandao wa facebook umetangaza kuwa unatafuta mbinu mpya ya kupunguza machungu unayopata wakati unapokutana na mpenzi wa... [Read More]

Kwa mara ya 3 kwa mwaka huu rapper mmiliki wa Young Money Lil Wayne, anakumbana tena na mkono wa sheria kujibu mashtaka yanayomkabili.

Sahau kuuhusu mashtaka ya Private Jet na kutolipa ‘bills’, safari hii bosi huyu anashitakiwa na ‘modo’ wa kike aitwae Shanise Taylor kwa kutumia picha yake katika moja ya tisheti zake kinyume na makubaliano.

Kwa mujibu wa TMZ Shanise amesema alipiga picha hiyo mwaka 2011 na kampuni ya mavazi ya Trukfit, ila hakusaini makubaliano kuwa picha yake itumike katika tisheti ambayo amemuona nayo Wayne.

Dada huyo anaishutumu pia kampuni hiyo kwa ‘kuedit’ picha yake, na kumuonesha kana kwamba ‘amesaula’ nguo zote hata ‘nguo ya ndani’ hana.

Anasema amedhalilishwa kwa hiyo anataka nguo hizo ziondolewe sokoni, lakini pia alipwe mkwanja utakao mpooza machungu yake.

LIL WAYNE KUSHTAKIWA TENA

Kwa mara ya 3 kwa mwaka huu rapper mmiliki wa Young Money Lil Wayne, anakumbana tena na mkono wa sheria kujibu mashtaka yanayomkabili. Sah... [Read More]

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini,Quick Rocka ameitaka serikali kuelewa na kuweka mkazo zaidi kuendelea sanaa ya Tanzania na kuifanya kuwa sehemu ya mapato ya nchi.

”Muziki au sanaa kwa ujumla ni kitu ambacho serikali ikiwekea mkazo kwamba tunafanya kazi kuna kulipa kodi,itaingiza pato kubwa na kukuza uchumi wa nchi kama ikichukuliwa kama kazi vijana wengi wamejiajiri kupitia sanaa za maigizo,muziki,uchongaji na uchoraji,ni vitu ambavyo watu wanapenda kufanya”,alisema Quick Rocka.

QUICK ROCKA AITAKA SERIKALI KUWEKA MKAZO JUU YA UKUAJI WA SANAA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini,Quick Rocka ameitaka serikali kuelewa na kuweka mkazo zaidi kuendelea sanaa ya Tanzania na kuifany... [Read More]

Mkali wa muziki wa Bongo Flava Seif ‘Matonya’ shaaban, ameuelezea wimbo wake wa ‘kitambo’ Vailety kuwa ndio wimbo uliompatia pesa nyingi kwa haraka.

Akizungumza jana kupitia kipindi cha ‘The Jump off’ cha Times FM, Matonya anasema wiki kadhaa tu baada ya kuiachia ngoma hiyo, alikutana na ‘mpunga’ mkubwa kwenye akaunti yake Benki.

“Vailety aisee was crazy song kiukweli, ulikuwa wimbo mkubwa sana, nilipokea simu nyingi kutoka Marekani na kwenginepo, yani ulipagawisha watu kiukweli.

Sasa sikuwahi kushika hela nyingi yani, pesa zangu nyingi zinaingia benki tu, sasa ile siku natazama akaunti naona kama milioni 150 hivi afu kwa haraka tu yani” alisema Matonya.

Katika ‘line’ nyingine, Tonya Time alikiri kuwa ‘mkwaju’ huo ulimpatia maadui wengi sana.

'VAILETY' YAMUINGIZIA MATONYA MILIONI 150

Mkali wa muziki wa Bongo Flava Seif ‘Matonya’ shaaban, ameuelezea wimbo wake wa ‘kitambo’ Vailety kuwa ndio wimbo uliompatia pesa nyingi k... [Read More]

MSANII wa muziki wa Bongo Flava Richard Mavoko, amesema kama asingekuwa mwanamuziki basi angekuwa mchezaji mpira mkali sana.

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Hatua Tatu’,Timesfm,  wakati akitambulisha ‘ngoma’ yake mpya ‘Ninaimani’ Rich anasema aliwahi kupelekwa mpaka shule ya ‘Vipaji’ Makongo kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata ‘kabumbu’.

“Unajua mi nilifaulu second selection, kwa hiyo wakati nipo nyumbani Mkuu wa shule kipindi hicho mzee Kipingu akanipeleka pale Makongo kwa kuwa nilikuwa najua sana kucheza mpira.

So matokeo yalivyotoka yapili yale, ikabidi nichukuliwe pale nipelekwe shule niliyofaulia Mnazi mmoja” alisema Mavoko.

RICH MAVOKO KUGEUKIA SOKA?????

MSANII wa muziki wa Bongo Flava Richard Mavoko, amesema kama asingekuwa mwanamuziki basi angekuwa mchezaji mpira mkali sana. Akizungumza k... [Read More]

MwanaHipHop maarufu nchini ‘Joh Makini” ambaye amekuwa gumzo baada ya kuachia video yake ya don’t bother,amesema analazimika kutumia gharama kubwa katika video zake anazofanya,ili azidi kujitangaza kwenye soko la muziki kimataifa.

Joh Makini alisema kwa sasa ameshafika hatua ya kimataifa,hivyo ni lazima afanye video zenye hadhi ya kimataifa.

Kwa hatua ambazo naenda natakiwa kulipa fedha kubwa katika video,gharama ya don’t bother ni zaidi ya Tsh milioni 20.7,hapo hauja ongezea manunuzi ya mavazi na vingine.

Joh amesema video hiyo imemfanya kuvunja rekodi ya video zote alizofanya na kuzidi kumtengenezea njia nzuri.

Pamoja na hayo,Joh Makini ameizungumzia kolabo yake na Davido ambayo inatarajiwa kutoka siku za hivi karibuni.

JOHN MAKINI KUJIGHARAMIA KIMATAIFA

MwanaHipHop maarufu nchini ‘Joh Makini” ambaye amekuwa gumzo baada ya kuachia video yake ya don’t bother,amesema analazimika kutumia ghara... [Read More]

Msanii wa muziki wa kizazi kpya nchini,Benald Paul ‘Ben Pol’ amesema ushiriki wake katika onesho la Coke Studio ni moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki.

Kauli hiyo aliitoa wiki hii kuhusu ushiriki wake kwenye onesho hilo linaloendeshwa na kampuni ya CocaCOla kwa kushirikisha wanamuziki wa Tanzania na nje ya nchi ambao wamekuwa wakifanya onesho la kuvutia.

alisema anajivunia ushiriki wake katika maonesho hayo na amefanikiwa kujifunza mengi kuhusu fani ya muziki.

Alisema anajisikia fahari kufanya kolabo kwa kushirikiana na wanamuziki wengi kutoka Kenya katika msimu huu wa Coke studio ambapo kwa hapa nchini onesho hilo linarushwa kila Jumamosi.

Ben Pol alisema onesho ka Coke Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonesha vipaji vyao na aliwataka vijana wenzake kujiamini na kutokata taaa iwapo wataka kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.

BEN POL: "COKE STUDIO NI HATUA KUBWA KWANGU KIMUZIKI"

Msanii wa muziki wa kizazi kpya nchini,Benald Paul ‘Ben Pol’ amesema ushiriki wake katika onesho la Coke Studio ni moja ya mafanikio katik... [Read More]

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging