Google PlusRSS FeedEmail

Muongozaji na mwigizaji nyota wa filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ amewaasa wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu kuwa wasitukane wakongwe waliopigania tasnia hiyo, leo tasnia inatolewa macho na kila mtu na kutoa ajira kwa watu mbalimbali hata Serikali imeliona hilo.

“Tasnia hii watu waliisusia ilikuwa ikionekana kama ni kazi ya ziada tu wala si kazi inayomwezesha mtu kuendesha maishayake, katika hali ngumu tulipigana na kufikia hapo ilipo ni kwa juhudi za wasanii pekee hawa ambao leo unaweza kuwabeza kwa sababu tu upo nao nawe unauza filamu zako,”anasema Ray.

Ray anasema kuwa katika kuhakikisha kazi zinakuwa bora kila mara utumia muda mwingi katika kuongeza vifaaa vya kisasa sambamba na kutumia watu wenye ujuzi wa filamu, lakini bado anajua kuwa kuna watu ambao akiwa nao ujifanya kumsifia akiwapa kisogo tu umponda, anashauri vijana washindane katika kazi na sikupoteza muda kwa kuwabeza watu.

“Huwezi kumdharau mtu kama Ally Yakuti kwa kusema eti kazeeka kiuandishi, ni dharau na kusahau mchango wa watu walioifikisha tasnia ya filamu hapa ilipo bila kuwepo hao tusingefika hapa tulipo,”anasema Ray.

REY'AWAASA WASANII WANAOCHIPUKIA"

Muongozaji na mwigizaji nyota wa filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ amewaasa wasanii wanaofanya ... [Read More]Kibonzo cha siku

VIBWEKA KATIKA PICHA NA VIBONZO KUHUSU SWALA LA ESCROW

Kibonzo cha siku [Read More]

Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, Baby Madaha na Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ wamenaswa usiku wakila bata huku wakiwa kimahaba.

Tukio hilo lilinaswa na kamera ya paparazi wetu hivi karibuni kwenye pub moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali Inspector alionekana akiwa amemkalia Madaha huku wakipigana mabusu.

Baada ya paparazi wetu kujitokeza na kuanza kuwafotoa, Inspector ambaye ni mume wa mtu alishituka na kujinasua kutoka kwenye mwili wa mwanadada huyo.Alipoulizwa juu ya kile alichokuwa akifanya wakati ni mume wa mtu, Inspector alisema:

“Kaka kwani kuna kibaya gani tulichokuwa tunafanya, tupo hapa tunapanga mambo yetu ya muziki na wala hakuna ishu zaidi.”Baby Madaha kwa sasa haijulikani anatoka kimapenzi na nani ila Inspector Haroun ni mume wa Bahati ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2004 na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Nassir na Shadya.

BABY MADAHA NA INSPECTOR HAROUN WANASWA KIMAHABA

Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, Baby Madaha na Haroun Kahena ‘Inspector Haroun... [Read More]

Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua.

Kwa mujibu wa mganga huyo ameeleza siri nzito kuwa msanii huyo hutinga nyumbani kwa mganga huyo kwa ajili ya kuchukua dawa kwa ajili ya kujiongozea mvuto na kumnasa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum.

Alidai kuwa msanii huyo wa kike amekuwa akienda nyumbani kwa mganga huyo Mwananyamala jijini Dar es Salaam, kuchukua dawa kwa ajili ya kumnasa Diamond Platnum

MENINAH ATINGA KWA MGANGA KUMNASA DIAMOND

Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’a... [Read More]


Eshe Buheti mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2014/2015 tuzo za ZIFF na Action & Cut Views Choice Awards amefunguka kwa kusema kuwa wale wote ambao wamekuwa wakihoji kuhusu yeye kuwa ni mshindi kwa mwaka huu wasipoteze muda, habebwi na mtu bali uigizaji wake na muonekano wake.

Wengi ni waoga sana katika kushindana kwa sasa mimi ni Bora najua kuigiza na rangi nzuri inayokubalika katika kamera, na najua ninachofanya hakuna wa kunibeba ili niwe Bora ni uwezo ambao kila msanii anatakiwa atafute ubora katika kuigiza,”anasema Eshe.

Msanii huyo anasema anaweza kuwa amefaidika na mabadiliko ya tasnia ya filamu kwani wakati ambao waigizaji wengine walipokuwa wakifanya vizuri hakukuwa na utoaji wa tuzo hivyo anasema kuwa ni wakati ambao wa mabadiliko kuwa mwigizaji bora wa kike haina maana kuwa wengine si bora.

ISHE AJIMWAGIA SIFA KEM KEM

Eshe Buheti mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2014/2015 tuzo za ZIFF na Action & Cut Views C... [Read More]

    

Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika klabu yake ya Lina’s kisha ukapitia mtaa wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba kisha kuelekea kijiji cha Kyaikailabwa.

“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo.

Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni nyumbani. 


Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini.

“Palifunga kabisa, huwezi amini ule msururu wa magari ulianzia Bukoba mjini hadi Kyaikailabwa, magari yenyewe asilimia kubwa yalikuwa ya maana.“Marehemu alikuwa tajiri na baadhi ya marafiki zake pia walikuwa matajiri sasa ilikuwa ni balaa maana magari ya kifahari tupu yalipamba msafara huo.

                                          WAKATOLIKI WAKATAA KUMZIKA
Chanzo hicho makini kilidai kuwa, kutokana na mazingira ya kifo na watu waliokwenda kuomba misa ya msiba huo kutokidhi vigezo, viongozi wa kanisa katoliki walikataa kuongoza ibada ya mazishi.
Ilidaiwa kuwa waliokwenda kuomba misa hiyo hawakuwa na sifa za kiimani (hawakuwa wakatoliki) sambamba na kutotumia busara wakati wa kujieleza.


Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu. “Waliokwenda kuomba misa hawakuwa wakatoliki halafu mbaya zaidi hawakuwa na busara wakati wa kujieleza, mapadri wakawagomea kuongoza ibada hiyo,” kilisema chanzo.
Badala yake, inadaiwa kuwa ibada ya kumuombea marehemu iliendeshwa na wakristo wa Kilokole iliyofanyika nyumbani kwake.

TUJIKUMBUSHE
Marehemu Mtensa aliyeacha mjane na watoto kwa mkewe wa ndoa, alikutwa na umauti Novemba 18, mwaka huu saa chache baada ya kuzidiwa akiwa ndani ya gari lake akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyejulikana kwa jina la Jackline Hassan.


Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini. Kitendawili kingine kilichoteguliwa ni kuhusu msichana Jack, mwenye umri wa miaka 25, ambaye awali iliaminika kuwa ni mpenzi wake aliyekutana naye ghafla tu, lakini inasemekana alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa Mtensa na kwamba hata wakati flani alipokuwa akienda Uganda kuwaangalia watoto wake waliokuwa wakisoma huko, alikuwa akiongozana naye.

Aidha, stori nyingine kutoka huko zinadai kwamba polisi wamekuwa wakitaka kumuachia msichana huyo wakiamini hakuwa na kosa, ingawa hakuna taarifa zozote zilizokwishatolewa hadi sasa kuhusu uchunguzi waliofanya.

MAZISHI YA MMILIKI WA LINA'S CLUB BUKOBA

      Wananchi wakiwa barabarani kushuhudia msafara huo ukipita. “Msafara ulianzia mochwari ya Hospitali ya Bukoba, ukapita katika kla... [Read More]

INADAIWA msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mpenzi wake Msami wajikuta wapo katika ugomvi usiojulikana chanjo ni nini?, huku ikidaiwa alazimishwa kupiga kibao.

Inasemekana wawili hao wamepishana kiswahili katika video iliyozagaa mitandaoni inasikika sauti ya Irene akimlazimisha Msami kumpiga kibao.

Msami amekanusha kuwepo kwa ugomvi kati yao, huku msanii Irene Uwoya akikataa kuzungumzia jambo hilo.

HII MPYA YA IRENE UWOYA NA MSAMI

INADAIWA msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mpenzi wake Msami wajikuta wapo katika ugomvi usi... [Read More]Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square pamoja na kaka yao Jude Okoye,Jumatatu ya Nov 24 wamempoteza mzazi aliyebakia ambaye ni baba yao mzazi hii ni miaka miwili tangu afariki mama yao.

P-SQUARE WAMPOTEZA MZAZI WAO

Mapacha kutoka nchini Nigeria Peter Okoye&Paul Okoye P- Square pamoja na kaka yao Jude Ok... [Read More]

UZINDUZI WA TUZO ZA TAFA NEW AFRICA HOTEL

              Siku iliyokuwa ikisisubiriwa kwa hamu sana ilitimia siku ya Jumapili ya tarehe 23.November .2014 katyika ukumbi wa New Afri... [Read More]ANAITWA Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond. Alizaliwa saa kumi na moja jioni ya Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. Wazazi wake walimpa jina la Nasibu wakiamini ni la bahati.


Diamond aliongea hivi karibuni na safu hii ya Mjue Huyu ambapo aliweka wazi mambo mengi ya maisha yake. Diamond akiwa hajapata ufahamu, yaani bado mdogo, wazazi wake walitengana kwa sababu ambazo bado hazijawa wazi na baba yake kumuacha na mama.

Kufuatia hali hiyo, ilibidi mama yake ahamie kwa mama yake mzazi (bibi wa Diamond), Tandale Magharibi, Dar. Hapo ndipo yakawa makazi ya mama huyo na mwanaye.
Mnamo mwaka 1995, Diamond alianza elimu ya awali katika Shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale- Uzuri. Mwaka 1996 alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Tandale- Magharibi iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mwaka 2000, Diamond akiwa darasa la tano alianza kupenda muziki, hivyo akawa anakopi baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wakihiti ndani na nje ya Bongo na kuimba yeye katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa kuliona hilo, mama yake alianza kumnunulia kanda za albamu za wasanii tofauti hata kumwandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi.

Diamond alizidi kuupenda muziki ikabidi mama yake awe anampeleka kwenye matamasha mbalimbali ili mwanae apate nafasi ya kuimba.

Baadhi ya ndugu walimjia juu mama huyo wakidai anamharibu mtoto badala ya kumuhimiza masomo anamwingiza kwenye muziki ambao walidhani haukuwa na faida yoyote.'Diamond Platinumz'

“Kusema ukweli pamoja na yote hayo, hali ya maisha ilikuwa si nzuri kwa mama maana hakuwa na kazi ya maana wala vyanzo vikubwa vya fedha, hivyo ilibidi atumie kiasi kidogo alichokipata kutoka kwenye kodi ya vyumba viwili alivyopewa na bibi ili kunisomesha,” alisema Diamond.


CHUMBA KIMOJA NA MAMA
Diamond aliendelea kusema kuwa, kutokana na kupangisha vyumba viwili ilibidi yeye na mama yake kuhamia kwenye chumba cha bibi yake na maisha yakaendelea humo.


AMALIZA SHULE YA MSINGI
Mwaka 2002, Diamond alimaliza masomo ya elimu ya msingi lakini ili aende sekondari, mama yake alimwambia aachane na habari ya muziki azingatie masomo aweze kupata elimu itakayomsaidia mbele ya safari katika maisha.


AFANYA MUZIKI KWA SIRI
Nyota huyo aliendelea kusema kuwa akiwa sekondari, aliendelea kuimba muziki lakini kwa siri kubwa ili mama yake asijue.
Mwaka 2004, anasema alianza kuandika nyimbo zake mwenyewe kwa kuwa akili bado ilimwambia mafanikio yake yatapatikana huko.


AFANYA VIBARUA APATE PESA
Mwaka 2006, Diamond alimaliza elimu ya sekondari na kuanza kuimarisha ndoto yake ya kuwa mwanamuziki.


Alikuwa hana kazi ya kufanya nyumbani hivyo alianza kutafuta vibarua mbalimbali vya kumuwezesha kupata riziki ya siku. Miongoni mwa kazi hizo ni kuuza mitumba, kuweka mafuta kwenye magari (vituo vya mafuta), kupiga picha, kupigisha simu na kazi za kwenye viwanda mbalimbali.

ITAENDELEA

HII NDIO HISTORIA FUPI YA DIAMOND

ANAITWA Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond. Alizaliwa saa kumi na moja jioni ya Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana iliyop... [Read More]

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging