Wiki chache zilizopita nilipokea wimbo wa msanii chipukizi aitwaye KATOMA na wimbo unaitwa MAUMIVU ambao ameurekodia nchini Uganda na pia ameimba Kiswahili na Kiganda kwa asilimia kubwa..Baada ya kuupiga kwa wiki kadhaa hasa katika kipindi cha Uhuru Flava ya Uhuru FM alimpigia simu Mtangazaji wa kipindi hicho Soggy Doggy Ambaye naye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na aliomba kufanya nae mahojiano na mara baada ya kipindi hicho cha Radio,Mtangazaji huyo alipigiwa simu na watu wakiomba namba za simu za msanii akidhani labda ni mapromota, na jana msanii huyo kanipigia na kusema kuwa alifatwa na watu wa Idara ya Uhamiaji wakihoji uraia wake
Katoma aliniambia kuwa walimshikilia kwa muda na kisha kumuachia baada ya kuwapa uthibitisho kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Katoma mkoani Kagera na aliimba Kiganda ili kuweza kupanua soko la muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania...