Filamu ya Glamour The reality behind Dreams inaingia sokoni mwezi huu wa nne, filamu hii ambayo imetayarishwa na Javad Jefferji, inataraji kutikisa tasnia ya filamu kutokana na utengenezaji wake huku mtayarishaji wa filamu hii akiwa mahiri katika mambo haya ya filamu kwa miaka zaidi ya kumi na ni mshindi wa tuzo mbalimbali kwa Zanzibara na sehemu nyinginezo.
Filamu hii ni ya kipekee kwa sababu baada ya utafiti na uandishi wa script mtayarishaji huyu alitumia nafasi yake kwa kumleta muongozaji na muigizaji mahiri wa filamu kutoka nchini India, muongozaji huyu ambaye amejijengea sifa kutokana na ufanisi wake anaitwa Amitabh Aurora, mkurugenzi huyu wa kampuni ya ZG Film Production ya Zanzibar anajivunia elimu yake aliyopata Uk na kuanza kuitumia.
“Nimekuwa nikiitangaza Zanzibar katika masuala ya Utalii na kupewa tuzo na Wizara husika, lakini ukweli ni kwamba pia ninatangaza kazi za filamu za hapa nyumbani na nimetoa mchango kwa kila sekta niliyoshiriki kama vile Sauti za Busara, ZIFF, elimu yangu kama Cinemaphotographer niliipata nchini Uingereza nina uzoefu zaidi ya miaka 15, na leo hii nakuja na filamu hii, ni imani kuwa kila mtu atajua nini tunafanya” Anasema Javad.Katika filamu ambayo inaongelea binti Sofia alifanikiwa kwa sababu ya kazi ya mitindo imeshirikisha wasanii kama vile Mustafa Hassanali, Tecla Mjata, Edward chogula, Eva Issack, Bond bin Seleiman huku kukiwa na watu wenye majina katika nchi hii, ni filamu kali wala si ya kuikosa, filamu imetengenezwa na ZG Film Production chini ya mtalaamu Javad Jefferji.