PRO 24 DJ'S KUJA NA VIDEO MIXING NDANI YA TBC 1
Kwa kuonyesha uzalendo kwa kuwajali mashabiki wao Pro 24 DJ'S kila siku ya Alhamisi watakuwa wanakonga nyoyo za washabiki wao kwa kupiga muziki live wenye radha tofauti tofauti zinazopatikana ndani na nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania kupitia Televisheni ya Taifa (TBC 1) kuanzia saa nne usiku hadi saa saba usiku.Usiku huo utajulikana kwa jina la Video Mixing
Ikiwa ni moja ya wajibu wao kuwaburudisha watanzania sambamba na kukuza pamoja na kuutangaza muziki wa Tanzania ili uweze kujulikana kimataifa , wapenzi wa muziki huo maarufu Bongo fleva watashuhudia zikipigwa mfurulizo ndani ya lisaa la kwanza huku zikifwatwa na mfululizo wa ngoma nyingine ili washabiki wote waweze kupata ladha ya muziki tofauti
Usiku wa Video Mixing utafanywa sambamba na Dj Deea, Dj Micho, na Dj Calvin utaanza rasmi siku ya Alhamisi 13 mwezi huu