Google PlusRSS FeedEmail

BABA YAKE RIHANNA ABARIKI MAHUSIANO YA RIHANNA NA CHRIS BROWN




wakati mwanamuziki Rihanna hivi karibuni alitangaza kuwa yuko tayari kuachia albamu yake mpya , mwanamuziki huyo amekuwa kimya kuzungumzia uhusiano wake na Chris Brown. Hata hivyo baba mzazi wa Rihanna sio tu ametoa baraka zake kwa wawili hao kuwa pamoja, lakini pia amesema anataka kuona wawili hao wakioana.

Rihanna,24, ameripotiwa kumaliza tofauti zake na Chris Brown  japokuwa Chris bado yupo katika kipindi cha muangalizo baada ya kumdunda Rihanna mwaka 2008

Baba wa Rihanna Ronald Fenty hana kinyongo chochote na Chris Brown na amesema kuwa anatumaini wawili hao watafunga ndoa siku zijazo.

Akizungumza na gazeti la 'life $ Stlye' baba wa Rihanna alisema; "chochote kinachompa furaha Rihanna. Natumaini siku moja atafunga ndoa. Kila mmoja anampenda Chris kwani ni kijana bora."

"Familia yangu ilikuwa inampenda Chris Brown hata kabla hawajakutana nae Siku zote nilikuwa nikifikiri kuwa Chris Brown ana kipaji kikubwa,  ni mtu mwema na siku zote ananiheshimu."alisema baba yake Rihanna

Rafiki wa karibu na Chris Brown alielezea ni namna gani wapenzi hao wa zamani wamekuwa wakifurahi kwa pamoja siku za karibuni"Ni penzi la kweli ambalo lilikumbana na changamoto lakini kwa pamoja wamefanikiwa kuzishinda changamoto hizo. Walipitia wakati mgumu lakini sasa wamerudi pamoja na nafurahi kuwaona wana furaha." alisema rafiki huyo wa Chris Brown.

"Bahati mbaya sio kila mmoja amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kurudiana huku kambi ya Rihanna ikielezea wasiwasi wao kuhusu vitendo vya nyuma vya Chris Brown." aliongeza rafiki huyo.

Sitashangaa kama Rihanna na Chris watafunga ndoa ili kuwaonesha watu kuwa hawajali kinachozungumzwa na kwamba wanaweza kufanya wanachotaka." alimalizia kusema rafiki huyo wa Chris.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging