Msanii nyota wa kizazi kipya mwenye mvuto wa kipekee anayetamba na ‘swaga’ za R&B Bernady Poul ‘Ben Pol’ amekuwa kivuto kikubwa kwa baadhi ya mashabiki hususani wanawake na mabinti huku wengine wakitamani hata wapate muda wa kukaa naye na kuzungumza pamoja
Ben Pol amekuwa kivutio katika stage ya club bilicanas baada ya kufanya shoo ya nguvu iliyoandaliwa na Televisheni ya Taifa(TBC ONE) pamoja na Pro 24 Dj’s, inayokwenda kwa jina la Usiku wa Club baada ya kuimba wimbo wake ‘Nikikupata’, wimbo huo ulionekana umeibua hisia za akina dada waliohudhuria katika shoo hiyo huku kila mmoja akinga’ngania kupanda jukwaani kucheza naye wengine kumbusu kwa kuashiria kukubali kazi yake
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti mabinti hao, mmoja liyejulikana kwa jina la Amina Abdalh alisema kuwa amekuwa akivutiwa na kazi za msanii huyo kila wakati kwani anaimba kwa hisia na maudhuhi yaliyobebwa kwenye kazi zake zinaendana na maisha yao ya kila siku
“Nampenda sana Ben Pol kwani anajua kuimba mbali na hilo pia nampenda kwa sababu anamvuto wa hali ya juu na anavuti kila mahali, kwa msichana yoyote wa kileo lazima atavutiwa naye na atatamani kuwa naye” allisema
Kwa upande wake Ben Pol akizungumzia kupendwa kwake na ‘mademu’ alisema kuwa, kupendwa huko kumetokana na umahiri wa kazi zake na nyimbo zake zinazowagusa mabinti hao
Alisema kuwa anapoandaa kazi zake huwa anawaangalia mashabiki wake na pia anaiangalia jamii ni kitu gani wanachokitaka na wanachokikubali kwa wakati huo
“Huwa napenda sana kuwajali mashabiki zangu na si kwa wasichana kunipenda pia napendwa na wasanii wenzangu kwa kuwa nao karibu na kushirikiana nao katika kazi zao” alisema Ben Pol
Ben Pol ambaye amepata tuzo ya wimbo bora wa R&B wa mwaka 2011/2012