LULU AHOJI JALADA LA KESI YAKE LILIPO
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayekabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba jana amehoji mahakamani na kutaka kufahamu jalada la kesi yake lilipo
Baada ya kuuliza swali hilo, Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao alimjibu msanii huyo kwamba jalada lake halisi lipo mahakamani hapo. “Mshitakiwa anauliza jalada gani halisi au, kama jalada halisi hili hapa “ alijibu wakili Sekwao
Mshitakiwa huyo aliuliza swali hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Stuart Sanga kwa kuwa kesi hiyo iliwahi kutajwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa kazi kutokana na Lulu kupitia mawakili wake waliwasilisha ombi Na 46/2012 chini ya hati ya dharura iliyokithiri Mahakama Kuu
Lulu na mawakili wake walikuwa wakiomba mahakama hiyo ya juu iamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,kulishunghulikia ombi la msanii huyo lililokuwa likiomba kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya watoto kwa sababu mshitakiwa huyo ana umri wa chini ya miaka 18
Baada ya mshitakiwa kujibiwa, wakili aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 5, mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika