Google PlusRSS FeedEmail

M.I.A, LADY GAGA WAZIKA 'BIFU'




M.I.A. na Lady Gaga wameweka kando tofauti zao na kuleta amani baina yao ,Rapa wa wimbo 'Paper Planes'alitengeneza vichwa vya habari baada ya kumchana nyota huyo wa pop katika mahojiano na jarida la NME mwaka 2010, "Anajitengeneza kwa staili ya Grace Jones na Madonna lakini muziki wake ni wa kitoto mno," aliliambia jarida hilo

"Si mtu anayepiga hatua ila ni mzuri wa kuigiza, anazungumza kama mimi hadi kunizidi"
Lakini licha ya madongo hayo M.I.A. alimualika Gaga kumtembelea mwazilishi wa mtandao wa WikiLeaks, Julian Assange wakati wa ziara yake ya jijini London wiki hii

"Kama uko Harrods leo njoo kumtembelea Assange katika ubalozi wa Ecuador, niko hapa nitakupa chai na keki" aliandika mwanaharakati huyo wa Sri Lanka

Gaga alifika mahali hapo na kumshangaa M.I.A "yaani nimepagawa asante kwa kuja ninafuraha kwa mba unaweza geuza bifu hizo za kwenye vyombo vya habari na kufanya vitu chanya " aliandika Maya

Lady Gaga anaye aliandika @mia universe umesema la maana bila shaka mimi na wewe tunaweza kuleta amani kwa manufaa ya wengine.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging