Jina lako halisi ?
Ben Pol: Naitwa Bernad Pol Mnyelange
Jina la Ben Pol umelitoa wapi?
Ben Pol :jina hili ni kifupicho cha jina langu halisi, na ninapenda kulitumia jina hili kwa ajili ya kunitambulisha mimi msanii pamoja na kazi zangu
Ni mwenyeji wa Mkoa gani ?
Ben Pol : Ni mwenyeji wa mkoa wa Dodoma, nimezaliwa Dodoma
Unafanya muziki wa aina gani ?
Ben Pol : Nafanya muziki wa R&B na hata ikitokea nikifanya muziki mwingine basi lazima utakuwa na mahadhi ya R&B kwa sababu ndio muziki ninaoupenda na pia ndio ninaoushabikia sana
Ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?
Ben Pol : Ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne
Kiwango chako cha elimu ?
Ben Pol : Nimesoma elimu yangu ya secondary katika shule ya Dar es salaam Secondary school mwaka 2004-2007,nikajiunga na elimu ya kitado cha tano katika shule ya Azania 2008-2009 , sasa nachukua Diploma ya Bank and Finance katika chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
Umeshatoa Albamu ngapi mpaka sasa?
Ben Pol : Nimetoa albamu moja mpaka sasa, ingawa kwa kipindi hiki nipo jikoni kuipika albamu yangu ya pili ambayo hivi punde itakuwa hewani, ambapo itaitwa 'Ben Pol'
Kwa nini umeamua kuiita albamu yako ya pili 'Ben Pol'
Ben Pol: Nimeamua kuipa jina la Ben Pol albamu yangu ya pili kwa sababu ninaisimamia mwenyewe kuanzia garama za kwenda studio mpaka kumfikia (mlaji) mshabiki wangu
Albamu yako ya kwanza uliifanya na nani?
Ben Pol :Albamu yangu ya kwanza niliifanya na Music Lab studio
Kwa nini umeamua kufanya albamu ya pili mwenyewe?
Ben Pol : Nimeamua kusimama mwenyewe kwa sababu sasa ninajimudu na nina mtaji wa kutosha kuingia studio na pia ni njia ya kujikuza kwenye tasnia hii ya muziki
Kilitokea nini kwenye albamu yako ya kwanza?
Ben Pol :Wakati naanza kufanya muziki sikuwa na mtaji wala mashabiki ila studio ya Music Lab walikiona kipaji changu na waliamua kufanya kazi na mimi na wamenifikisha hapa nilipo
Mafanikio uliyoyapata yaliyotokana na albamu yako ya kwanza?
Ben Pol : Kuweza kujisomesha chuo na kujilipia ada ya chuo bila tatizo lolote, huku nikiwa na uwezo wa kuyaendesha maisha yangu bila ya kuwa tegemezi, pia nimeweza kupata mashabiki wengi, ambao wamenisababisha niweze kupata tuzo ya Kill Music Award's
Umepata tuzo ngapi?
Ben Pol : Nimepata tuzo mbili za mwimbaji bora wa R&B 2011-20012 na nyimbo zilizonipa ushindi ni 'Nikikupata ' pamoja na My number One fun
Ni kitu gani unachokikumbuka katika maisha yako?
Ben Pol :Siku niliyopokea tuzo ilikuwa siku ya kipekee sana na huwa ninaikumbuka kwani ilikuwa ni siku ya firaha hata kama ukikumbuka nilishindwa kuongea siku hiyo nilipokuwa nakabidhiwa tuzo yangu
Ni kitu gani unachukia sana ?
Ben Pol : Nikiona mtu anavujwa moyo huku akinyimwa nafasi ya kuonyesha kile alichokuwa nacho huwa ninaumia na kuchukia pia
Ni kitu gani unachopenda kuvaa na ukikikosa huwa unajihisi tofauti?
Ben Pol : Napenda sana kuvaa miwani kwani nahisi inanifanya nizidi kupendeza na kuongeza muonekano wangu kuwa na mvuto zaidi
Ni sehemu gani ya mwili wako unahisi unamvuto?
Ben Pol : Sina uhakika sana ila nahisi sauti yangu inamvuto sana
Huwa unaandika mwenyewe mashahiri yako ?
Ben Pol: Huwa naandika mwenyewe nyimbo zangu na nyingine pia nawaandikia watu hususani wasanii wachanga
Ushamwandikia msanii gani mpaka sasa?
Ben Pol : Nimeshamwandikia msanii chipukizi kutoka THT mpaka sasa
Ni kitu gani kitatushangaza kuhusu wewe?
Ben Pol : Naweza nisitoke nje nikashinda nyumbani tena chumbani hata siku tatu nikiwa nasikiliza muziki