Google PlusRSS FeedEmail

DOTNATA ATOA BARAKA



Mwigizaji mkongwe wa kike katika tasnia ya filamu za kibongo, ambaye pia ni mjasiriamali Husna Posh 'Dotnata', kwa sasa amegeukia sanaa ya muziki wa nyimbo za injiri na kuiacha nyimbo yake inayokwenda kwa jina la  Baraka

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Dotnata alisema kuwa ameiachia nyimbo ya baraka kati ya nyimbo mbili ambazo teyari amesharekodi na yuko mbioni kuziachia hivi karibuni ili jamii iweze kutambua nini kilichomo katika nyimbo hizo

Alisema kuwa ameamua kuwashirikisha wasanii chipukizi wawili wa kike katika nyimbo hiyo ili kukuza vipaji vya wasanii katika upande wa nyimbo za injiri

"Kwa sababu nyimbo inaitwa baraka nimeamua kuwashirikisha wasanii wa kike ili baraka zianze kwa wakina mama kwanza, na pia ni katika hali ya kukuza vipaji vya wasanii kwenye upande wa nyimbo za injiri" alisema Dotnata

Alisema kuwa uwezo aliouonyesha kwenye nyimbo hiyo ni mkubwa sana ,huku akisisitiza kuwa nyimbo hiyo imebeba maudhuhi ya hali ya juu yanayoendana na jina lenyewe la baraka hivyo aliwaomba watanzania waipokee nyimbo hiyo na waifanye ya kwao ili wapokee baraka hizo

Aliongezea kuwa nyimbo hiyo ambayo teyari ameshatoa video yake, na teyari imeanza kupigwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari aliwataka mashabiki wake wakae teyari kuzipokea nyimbo nyingine ambazo hivi karibuni ataziachia



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging