Hali ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Rehema Chalamila (Ray C) inaendelea kutengama baada ya kuendelea kupata matibabu na huduma muhimu kwa watu wake wa karibu akiwemo Ruge Mtahabwa
Hali yake kiafya ilibadilika baada ya kutumia madawa ya kulevya kwa wingi ambapo ilisababisha kupoteza dila yake nzima ya maisha yake kiujumla
Akizungumzia swala hilo Mkurugenzi wa Nyumba ya kukuza Vipaji (THT) Ruge Mutahaba alisema kuwa hali ya msanii huyo kwa sasa inaridhisha kwa kupatiwa huduma ya karibu ikiwemo ushauri ili iweze kurudi katika hali yake ya kawaida
Alisema kuwa kwa upande wake yeye anatoa mchango mkubwa kwa msanii huyo ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kufanya vizuri katika kazi zake za muziki
Ruge alisema kuwa wasanii wengi wanajikuta wanaingia katika maswala ya ulevi na kubwia unga kwani inatokana na kukosa muongozo mzuri katika maisha yao pamoja na shughuri zao za kimuziki
"Msanii atasikika na nyimbo zake jina litakuwa kubwa lakini matokeo yake wanaingia katika matumizi ya madawa ya kulevya ni kwa sababu ya kukosa muongozo na ushauli mzuri wa kuwaongoza katika maisha na kazi zake"
Ruge aliongezea kuwa msanii mzuri ni lazima ume na kiongozi mzuri kwa ajili ya kuongoza kazi zako pamoja na kuwa na mtu mzuri wa masoko ili uweze kufanya vizuri kimasoko hususani kwa nia ya kufika kimataifa