LIL SCRAPPY ATAKA SHERIA YA BANGI IWEKWE WAZI
Rapa Lil Scrappy, ameungana na wasanii wengine kutaka sheria za jimbo lake la Atlanta za kuzuia uvutaji bangi iondolewe
Rapa huyo alisema "itakuwa bomba ile mbaya kama bangi itaachiwa kuvutwa huru kama inavyofanywa kwa baadhi ya majimbo nchini humu" alisema na kuongeza kuwa
"Nilifurahi sana wakati nilipokuwa Colorado, nilipokuwa naelekea katika shoo nilivuta kwanza na hakuna sheria inayomzuia mtu kuvuta" aliongezea kuwa "tunahitaji sheria hii ya kuruhusu uvutaji bangi itumike pia Atlanta
Wasanii wengine waliounga mkono kauli hiyo ni pamoja na Cash Out aliyesema "naunga mkono sheria hiyo itambulike kisheria kinachotakiwa ni kuruhusiwa kutumika kila mahali ili kila mmoja afurahie maisha katika nchi hii