Jina lako kamili :
Linex : Naitwa Sunday Mseda Alias
Jina lako la utoto?
Linex : Nilivyokuwa mtoto walikuwa wananiita Sunday bishoo kwa sababu nilikuwa napenda sana kucheza mpira kwa mapozi sana na kwa fujo hadi marafiki zangu walikuwa wananichukia kwa sababu ya kutumia rafu sana kwenye mpira wa miguu
Safari yako ya muziki tangu utotoni ikoje?
Linex : Nimezaliwa katika familia ya muziki mama zangu wote wanaimba kwenye upande wa nyimbo za injiri hivyo hata familia yangu haikushangaa mimi kuwa muimbaji, na nilikuwa nipo nao bega kwa bega katika kazi hizo ya muziki nilijikuta naanza kuimba taratibu mpaka sasa
Safari yako ya muziki kwa kipindi hiki kabla haujajulikana ilikuwaje?
Linex : Nilikuwa napenda sana kutembelea bendi na nilikuwa nafanya mazoezi kwenye bendi mbalimbali za muziki na zilinipa changamoto sana mpaka hapa nilipo sasa
Muziki ulianza lini?
Linex : Nilianza muziki rasmi mwaka 2005
Nyimbo gani ilikutambulisha katika gemu ya muziki?
Linex : Nyimbo iliyonitambulisha katika gemu ya muziki ni Mama Halima kwani mashabiki pamoja na wadau wa muziki walihisi mimi siyo mtanzania kwa mtindo niliyokuwa nimeutumia katika nyimbo hiyo
Umeshatoa jumla ya albamu ngapi?
Linex : Mpaka sasa nimetoa albamu moja ingawa nina albamu zaidi ya tano, siwezi kutoa nyingine kwani albamu hazilipi nitakuwa ninatoa single tu kwa ajili ya kutambulisha muziki na biashara kiujulma
Kwa nini unapenda kuimba nyimbo za hisia?
Linex : Napenda kuimba nyimbo za hisia kwa sababu nyimbo zangu zinatoka ndani ya moyo wangu, siwezi kuimba uongo, hivyo ninachokiimba ni kile kinachotendwa na watu wengi kwenye jamii, mfano mtu unayempenda utazungumza naye kwa hisia kubwa
Nini matarajio yako ya baadae?
Linex: Ni kuwa msanii mkubwa wa Afrika kwa sababu uwezo na nia ninayo na kuhakikisha malengo yangu ninayafanyia kazi ni pamoja na kujitahidi kutafuta nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika
Msanii gani wa Bongo anayekuvutia?
Linex : Wasanii wote wa bongo ninawapenda na wananivutia kikubwa ni kwamba yule anayefanya kazi yake vizuri kwangu mimi ni msanii bora
Kazi gani ya msanii unaipenda kuisikiliza kila mara?
Linex : Napenda kuisikiliza kazi ya msanii kutoka South Africa Zahara kwa sababu anaimba kama mimi kazi zetu zinafanana hicho ndio kikubwa kinachonivutia kusikiliza nyimbo zake
Kazi gani ya muziki kwako ilikuwa ngumu?
Linex : Ngwekewa ilikuwa kazi ngumu sana kwangu na ilinichukua muda mrefu sana kuikamilisha hususani kwenye upande wa video ilinichukua siku nne kuikamilisha kazi hiyo kwangu
Unauzungumziaje kila mtu kujiingiza katika tasnia ya muziki?
Linex : Uzuri wa sanaa haudanganyi na kizuri kinajionesha na bahati nzuri sasa watanzania wanajua kipi bora hivyo kila anayejiingiza katika tasnia hiyo azipokee changamoto hizo huku ahakikishe kuzifanyia kazi
Ni muda gani unaotumia kutunga nyimbo zako?
Linex : Mimi siafanyi muziki wa kutamba leo kesho ukapoteza ladha hivyo muda wangu mwingi huwa nafikilia muziki gani unaendana na misha halisi ya binadamu, kama nilivyokwambia muziki wangu unatoka moyoni hivyo ndivyo ninavyofanya kupata nyimbo bora, napata nafasi ya kujirekodi mwenye nyimbo kwanza kabla ya kuingia studio
Njia gani unatumia kupata jina la wimbo
Linex : Sijawahi kupata jina la wimbo wkati natunga nyimbo,nyimbo yangu ikishahisha ndipo jina linakuja
Unatumia kilevi chochote?
Linex : Situmii kilevi chochote kile na wala madawa ya kulevya situmii
Mahusiano gani yaliyokutesa sana?
Linex : Mahusiano yaliyonitesa sana nikwamba nilikuwa na mahusiano lakini umbali ndio lilikuwa ni tatizo kwetu na tuliachana kwa sababu hiyo, kwa upande wangu iliniwia vigumu sana kwa kuachana na mtu niliyekuwa nampenda kwa sababu ya umbali
Kazi gani unafanya tofauti na Muziki?
Linex : Mimi ni mfanyabiashara mdogo ninajihusisha na maswala ya biashara