RADO AJA NA 'MADUHU' KWA AJILI YA KUMUENZI MAREHEMU KANUMBA
MSANII anayetamba katika tasnia ya filamu nchini ambaye pia ni muandaaji wa filamu Saimon Mwapagata 'Rado' anatarajia kuachia filamu yake hivi karibuni inayokwenda kwa jina la 'Maduhu' akiwa amewashirikisha wasanii chipukizi ambao walikuwa wakifanya kazi na Marehemu Steven Kanumba akiwa na dhumuni la kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto hao
Akizungumza na jalida hili la Maisha alisema kuwa filamu hiyo ambayo anaamini kuwa itakuja kuleta mabadiliko makubwa katika soko la filamu pamoja na kubadilisha fikra za watanzania wengi kwa sababu ya maudhuhi yaliyobebwa ni halisi na yanaendana na mazingira halisi ya nchi yetu
Alisema kuwa filamu hiyo ambayo inaelezea tofauti ya malezi wanayoyapata watoto hasa wazazi au mlezi anapofariki kwani huwaacha watoto hao wakinyanyasika na baadhi yao kukosa muelekeo wa maisha
Rado alisema kuwa ameamuwa kuwachukuwa watoto walikuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kwa ajili ya kupata uhalisia na kuonyesha jamii kuwa pengo aliloacha marehemu huyo haliwezi kuzibika
Aliongezea kuwa ameamuwa kutengeneza filamu hiyo kwa ajili ya kukuza na kumuenzi marehemu Kanumba kwa kuendeleza vipaji ambavyo alikuwa anandoto na malengo ya kukuza tasnia ya filamu kwa ujumla ndani na nje ya nchi
Alitoa wito kwa mashabiki kumuunga mkono kwa kununua copy halali za filamu hiyo ili kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuezesha kazi ya filamu iendele nchini