SANZA PROFILE
Unaitwa nani?
Sanza : Naitwa Sanza Mukajanga
Unaishi wapi?
Sanza : Naishi Mbezi Beach
Chakula Gani unapendelea?
Sanza : Napenda Ndizi Kuku
Unapenda kufanya nini ukiwa umepumzika?
Sanza : Napenda kusikiliza muziki na ndio kitu ninachokipende sana, kwani naamini muziki ni dawa na ukiiutumia vizuri muziki unakufariji na unapona
Rangi gani inayokuvutia?
Sanza : Napenda rangi nyekundu na huwa nikivaa inanifanya nivutie zaidi
Elimu yako?
Sanza : Nina elimu ya chuo kwa ngazi ya shahada
Kuwa mwanamitindo ulianza lini?
Sanza :Nilianza kuwa mwanamitindo tangu niko mtoto kwani mama yangu alikuwa ananiambia nilikuwa nachagua nguo kulingana na wakati na mazingira hivyo hali hiyo imenisababisha nikuo huku nikijiona ninafaha kuwa mwanamitindo
Matarajio yako ya hapo baadae?
Sanza : Baada ya miaka 3 kuwa mwanamitindo wa kimataifa huku nikiipeperusha benda ya nchi yangu vizuri katika ulimwengu wa mitindo
Ushawahi kufanya kazi na kampuni yoyote ya mitindo?
Sanza : Ndio nimeshawahi kufanya kazi na Asia kwenye kampuni ya Fabic Fashions
Ushawahi kushiriki mashindano yoyote ya urembo nchini?
Sanza : Nimeshawahi kushiriki Miss Dar City Collegy, na Miss Ilala
Matokeo ya Miss yalikuwaje kwa upande wako?
Sanza : Kwa upande wangu yalikuwa ni matokeo mazuri kwani kwa upande wa wilaya ya ilala nilifanikiwa na kuingia katika ngazi ya Dar City Collegy hivyo matokeo yalikuwa vizuri bila ya upendeleo
Unahisi wewe ni mrembo?
Sanza : siyo tu kuhisi ila najua kuwa mimi ni mrembo na ninavutia pia
Unapenda kitu gani katika mwili yangu?
Sanza : Napenda miguu yangu sana katika mwili wangu na ndio maana napenda kuvaa nguo fupi ili miguu yangu ionekane
Unahisi wavulana wanababaika na urembo uliokuwa nao?
Sanza : Walikuwa wanababaika sana na kunisumbua hapo mwanzo ila sasa wameshanizoea wananiheshimu hicho ndio kikubwa sana kwangu