TONI BRAXTON APIGA BEI NYUMBA YAKE
MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya R&B Toni Braxton amemua kupuga bei nyumba yake ya kifahari kwa dola 1.1 milioni.
Braxton amefikia hatua hiyo kutokana na madeni anayodaiwa kutoka mwaka 2004 mpaka 2010.
Kuna wakati nyumba moja ya msanii huyo ilitaka kupigwa mnada kutokana na madeni lakini mahakama ilimuachia kutokana na madai kutokamilika.
Nyumba hiyo yenye ukubwa wa mita 11,400, ina vyumba sita vya kulala, mabafu sita ya kuoga, chumba cha kusomea na jiko.
Hiyo itakuwa nyumba ya pili kuuzwa na Braxton aliyewahi kutamba na kibao chake cha An Break my Heart.