Wasanii nchini washauriwa kutumia mfumo wa digital ili kujenga msingi wa muziki wa kibiashara wa kimataifa huku wakisahau matumizi ya stika kwani siyo pekee zitakazo weza kukuza muziki na kufikisha malengo ya wasanii wengi katika ngazi ya soko la kimataifa
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT) Ruge Mutahaba katika kuwasilisha mada jukwa la sanaa (BASATA) jana jijini Dar es Salaam alisema kuwa wasanii wengi hawajui thamani yao na umuhi wa matumizi ya mfumo wa digital kwa nia ya kujiuza katika soko la kimataifa
Alisema kuwa wadau wa muziki na wasanii wenyewe wanatakiwa kufahamu kuwa CD hazina nafasi tena katika soko la kimataifa hivyo wanatakiwa kujiimarisha zaidi na kujitangaza katika masoko ya ulimwengu kwa kutumia mfumo wa digital
Alisema kuwa elimu inatakiwa itolewe kwa wasanii wote ili kujua umuhimu na thamani yake na njia zipi za kupita ili afike huko anakotaka kufika ili kutimiza malengo yake ya muziki kwa kuukuza na kujitangaza katika soko
Ruge alisema wasanii waache dhana ya kufanya kazi peke yao kwani kwa kufanya hivyo matokeo yake wanashindwa kufikisha malengo yao matokeo yao wanabaki kulalamika kila siku na malalamiko yao hayajengi chochote zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo yao
Ruge aliongezea kuwa wasanii wanatakiwa kupewa pia elimu juu uelewa wa call tune ambapo matokeo yake wananufaika watu wachache na wasanii hao kubaki maskini
Alisema kuwa kila msanii ajue haki yake ili aweze kuisimamia haki hiyo pia waache kulalamika na matokeo yake wajifunzi vitu vitakavyo wajenga ili kujikuza kisanaa na jinsi ya kujiongoza katika kazi zao