JB KUFUNGA MWAKA NA FIKRA ZANGU
MSANII anayetikisa katika kiwanda cha filamu nchini Jacob Steven 'JB' kufunga mwaka na filamu inayokwenda kwa jina la Fikira zangu ambayo amewashirikisha wasanii wenye majina huku akifungua mipaka zaidi kwa kucheza na msanii mwenye asili ya Uturuki
Akizungumza na jarida la Maisha JB alisema kuwa mwisho wa mwaka ndio wakati ambao anakuwa mwangalifu kwa kutoa kazi zenye ubora zaidi kwani ndio filamu zinazoacha kumbukumbu katika soko la filamu
"Filamu hii ni mahususi kwa mashabiki wangu waone nini nimekiandaa kwa kipindi cha mwaka mzima huwa ninafikiria sana kuwa na filamu yenye ubora zaidi mwisho wa mwaka ili kuwa na kumbukumbu kwa wadau na mashabiki wangu " alisema JB
Aliongezea kuwa siku zote huwa anatoa filamu zenye ubora lakini hii ya mwisho wa mwaka anaifanya ionekane tofauti kwani ni zawadi kwa mashabiki wake kwa kumuunga mkono kwa kipindi chote cha mwaka
Akizungumzia sababu zilizomfanya kucheza filamu hiyo na raia wa Uturuki alisema kuwa story ilikuwa inamuhitaji msanii wa namna hiyo hivyo ni sababu za kuboresha sanaa na kutafuta uharisia wa kitu husika
Alisema ujio wa filamu hiyo mwisho wa mwaka anaamini kuwa italete mapinduzi katika soko la filamu nchini kwa kuwa na ubora wa hali ya juu