TAFF WASHUKURU WADAU WA SANAA KWA 'SAPOTI'
Kutokana na watanzania pamoja na wadau wa sanaa kutoa ushirikiano wa kutosha katika matatizo yanayowapata wasanii nchini Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF)limewashukuru watanzania kwa kujitolea kuwasaidia wasanii waliokumbwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya maradhi na ushirikiano wao katika misiba ya wasanii waliofariki duniani hivi karibuni akiwemo Hussein Mkiete 'Sharomilionea'
Akizungumza wakati wa mkutano wa wasanii wa filamu jijini Dar es Salaam Rais wa Shirikisho Simon Mwakifamba aliwashukuru watanzania kwa kuunga mkono kwa jitihada zao katika kuwahudumia wasaniiwaliokumbwa na maradhi wakiwamo Juma Halfan 'Mzee Kankaa' Wagamba 'Mzee Small' na Juma Kilowoko 'Sajuki'
Alisema kuwa shirikisho hilo limeingia majonzi makubwa kutokana na vifo vya wasanii wake wakiwemo Steven Kanumba, Mlopelo, John Maganga na Sharomilionea