Google PlusRSS FeedEmail

BEN POL AJIVUNIA MAFANIKIO ALIYOYAPATA MWAKA 2012




MSANII anayekuja kasi katika miondoko ya R&B Bernald Pol 'Ben Pol'atambia mafanikio aliyoyapata kwa mwaka uliopita na kuwa na mikakati kambambe kwa mwaka huu kwa kuwa miongoni mwa wasanii watakao kuwa na uwezo wa kufanya shoo kubwa nchini

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ben Pol alisema kuwa mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wa mafanikio kwake kwa sekta ya muziki kwa kuwa na mashabiki wengi ambao wametambua kazi zake na kumpa ushirikiano kwa kipindi chote hicho

Alisema mafanikio hayo yamesababishwa na nyimbo zake alizotoa Pete, Maneno maneno pamoja na Samboira kufanya vizuri na kumuwezesha kupata shoo nyingi na kuweza kupata kipato kwa muda wa mwaka ulioisha

Ben Pol ambaye anaonekana kufanya vizuri katika fani hii ya muziki katika upande wa R&B alisema pia moja ya mikakati aliyoiweka kwa mwaka huu 2013 ni kuwa miongoni wa wasanii watakaofanya shoo kubwa nchi ili kudhihirisha mashabiki wake kuwa ana ubunifu wa kutosha na bado anauwezo wa kuendelea kubaki kwenye gemu hilo na kuendelea kufanya vizuri


Pamoja na hayo Ben Pol alitoa wito kwa serikali kuboresha njia za biashara katika soko la mauzo ya kazi za wasanii ili waweze kupata kipato na kujikwimu kimaisha

Alisema kuwa wasanii wengi wanashindwa kutoa albamu kwa kile kinachodaiwa kuwa albamu hazilipi hivyo serikali inatakiwa kusimamia njia na kuboresha ili wasanii waweze kujiendeleza katika kazi zao

Aliongezea kuwa muziki sasa umekuwa kwenye mpango wa biasha ra zaidi tofauti na kipindi cha nyuma kuwa mashabiki walikuwa wanavutiwa na kazi za sanaa na kujikuta matangazo ndio yanauza zaidi muziki tofauti na mara ya kwanza

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging