Kampuni ya bia Tanzania (TBL), wamesaini mkataba wa miaka mitano na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya kudhamini tuzo za muziki maarufu kama 'Kilimanjaro Music Awards'.Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema mkataba huo utagharimu shilingi 4 bilioni na kwamba kila mwaka tuzo hizo zitagharimu shilingi 800 milioni.Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mwaka 12 sasa, zimepangwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kutambua wasanii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.kwa niaba ya Serikali, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Lebejo alishukuru Kilimanjaro kwa udhamini wao kwa lengo la kukuza wasanii na kuwataka wasanii watakaoteuliwa kushiriki kwenye kinyang'anyiro hicho basi waheshimu uteuzi huo.