Rapa Lil Wayne aruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuimarika ambapo alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center
Baadhi ya vyanzo vya habari vimekanusha uvumi ambao uliokuwa umezagaa kuwa kulazwa kwake hospitalini kumechangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya
Ingawa rapa huyo ameripotiwa kutoka hospitali na ugonjwa wake hauna mahusiano wowote na matumizi ya madawa ya kulevya Lil Wayne anaonekana kuwa kwenye orodha ya wasanii wanaotumia madawa ya kulevya
Kama ambavyo ilishawahi kuripotiwa hapo awali kuwa rapa huyo alikubali kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya kwa kipindi cha miaka kadhaa na kuna taarifa kwamba ugonjwa wake huo umetokana na matumizi ya madawa ya kulevya
Pimp C huyu pia ni rapa pamoja na mtyarishaji wa muziki kutoka kwenye kundi la UGK pia ni mmoja wa wasanii wakubwa duniani ambaye pia ameingia kwenye orodha ya matumizi ya madawa ya kulevya
Baada ya kuachia albamu yake akiwa na umri wa miaka 33 mwili wa rapa huyo ulikutwa katika chumba cha hoteli jijini Los angeles, kifo chake kilitokana na kushindwa kupumua matatizo yaliyosababishwa na matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya
Whitney Houston
Mbali na kukanusha kutumia madawa ya kulevya hadharani kwa miaka kadhaa bado alikuwa akiripotiwa kutumia madawa ya kulevya mpaka umauti ulipomfika mwaka 2012