Katika tasnia ya mitindo kumekuwa na mazoea ya kuona mitindo mingi ya wasichana kama nguo, nywele, viatu, ila mbunifu Martni Kadinda ameweza kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia hiyo kwa kuwa mbunifu wa mavazi hususani kwa vijana wa kiume
Vibunduki ni aina ya mavazi ambayo yamebuniwa na mwanamitindo huyo ambayo ni maalumu kwa wanaume wanaoenda na wakati, ni aina ya suruali ambazo zinavaliwa bila mkanda ambapo unaweza ukavaa ukiwa umechomekea au kuchomolea upande mmoja
Akifafanua juu ya mavazi hayo Kadinda alisema kuwa ubunifu ni mmoja ya maisha yake hivyo anaamini kama suruali inamtosha hana sababu ya kuvaa mkanda na ndio maana alikuja na wazo la kubuni nguo za mtindo huo ambazo zinakuwa hazina sehemu ya kupitisha mkanda ila zinakuwa zinamtosha mvaaji
Alisema kuwa aina ya uvaaji huo unaweza kuvaa na shati ya aina yoyote pamoja na kuchagua rangi yeyeto ile ambayo unahisi inakupendeza na kukufanya uwe huru zaidi kwani wanaume huwa hapendi sana kuwa na machaguo ya juu zaidi huwa wanapenda kuonekana simple na nadhifu kila wakati
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.