MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego ameizungumzia nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Muziki gani' ambayo imekuwa gumzo kwa kipindi cha siku mbili kuwa ni kuwa na mikakati iliyo thabiti na kutaka kila mmoja kukubali kile anachokifanya na kuwa wabunifu katika muziki wa bongo fleva ili kupoteza dhana ya kutoa kazi zenye kufanana
Nyimbo hiyo ambayo imeimbwa na Ney wa Mitego pamoja na msanii anayetikisa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnam yenye mahadhi ya Hip Hop inayoenda kwa mtazamo wa kubishana baina ya waimbaji wa Hip hop na bongo fleva (wabana pua)
Akizungumzia nyimbo hiyo jijini Dar es Salaam Ney alisema kuwa chanzo cha nyimbo hiyo ni mtangazaji wa kipindi cha planent bongo ambaye alitoa wazo la wasanii hao kufanya nyimbo moja ikiwa na lengo la kuleta mapinduzi katika gemu ya muziki wa kizazi kipya
"Tulikuwa tumeandika nyimbo nyingine kabisa lakini baada ya mchizi kuisikiliza akatushauri tufanye kitu kingine na ndipo wazo la muziki gani lilipokuja sasa naamini watanzania wameielewa nyimbo hiyo" alisema Ney
Aliongezea kuwa ingawa nyimbo hiyo inatrambulika kama yake lakini kila mtu anahaki na uhuru wa nyimbo hiyo hivyo watanzania waipokee kwa mikono miwili iliwa inaimbwa na Diamond au na yeye popte pale
Aliongezea kuwa nyimbo hiyo anaamini kuwa italeta changamoto kubwa hususani kwenye gemu la bongo fleva hivyo aliwataka wanamuziki kuamini kile wanachokifanya pamoja na kuwa wabunifu katika muziki ili kuleta ushindani pamoja na kuwapa mashabiki kile kitu wanachokitaka huku wasanii wakiendelea kubaki kwenye muziki kwa muda mrefu bila ya kupotea