MSANII wa muziki wa kizazi kipya Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' ameanza kujitamba kwa kuwa na uhakika wa kunyakua tunzo za Killimanjaro music awards kwa kile anachokida kuwa ubora wa kazi zake ndio kitakachompa tunzo hizo
Kujitamba huko kumetokana na kazi zake kuonekana kupokelewa vizuri kwa mashabiki wake huku akiwa amevuka hatua kubwa kwa kupata shoo nyingi ndani na nje ya nchi
Alizungumza hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea maendeleo ya wimbo wake mpya alioufanya na mwanamuziki ambaye pia ni pruducer wa muziki kutoka nchini Nigeria Martins Justice 'Jay Martins' unaojulikana kwa jina la 'Tupo na Tunago" alisema anauwakika wa kuvunja rekodi katika tunzo za mwaka huu kwa kuwa na kazi zenye ubora ambazo zimepokelewa vyema na mashabiki wake
Alisema kuwa msanii yeyeto yule anayefanya kazi kwa juhudi lazima afikilie mafanikio yanayopatikana kutokana na matokeo ya kazi hiyo na kuongeza juhudi ili aweze kuboresha kazi zake
"Mimi nafuata njia zote za kuweza kunifanikisha kwa kile ninachokitaka ikiwemo kujituma na kuongeza juhudi katika kazi zangu huku nikizingatia kushirikiana na wasanii wenzangu kwani naamini kupitia wasanii wenzangu najifunza mengi" alisema Dimpoz
Akiizungumzia nyimbo yake msanii huyo alisema kuwa ameamua kufanya nyimbo hiyo kwa kushilikiana na msanii huyo kwa sababu ya kujitangaza na kutafuta soko la kimataifa
Kutokana na hilo aliweka wazi anaweza kupanda na kuongeza mashabiki wengi katika nchi za Afrika kwa kumtumia msanii aliyeshirikiana naye kwenye nyimbo yake huku akiwa na imani kuwa nyimbo hiyo itafanya vizuri katika soko la muziki nchini
Aliongezea kuwa kwa sasa wako katika mkakati wa kutafuta kampuni nzuri ili waweze kuboresha shooting ya nyimbo hiyo ambayo anaamini itakuwa yenye kiwango cha ubora zaidi ya kazi alizowahi kuzifanya hivyo kupitia kazi hiyo anaamini kupiga hatu zaidi katika kazi zake