Google PlusRSS FeedEmail

PROFESSOR JAY ATOA SOMA KWA KILL MUSIC AWARD




MSANII mkongwe wa miondoko ya  Hip Hop Tanzania Joseph Haule 'Professor Jay' amewataka waandaaji wa tunzo za Kilimanjaro music award kuboresha mchakato mzima wa kuwania tunzo hizo ili kuepusha malalamiko pamoja na hali ya sintofahamu kwa wadau wa muziki pamoja na wasanii

Akizungumza jijini Dar es Salaam msanii huyo alisema miaka ya nyuma mchakato wa tunzo hizo zilionekana kulalamikiwa na baadhi ya wasanii pamoja na wadau wa muziki kuwa zina mapungufu na kusababisha msanii kujishusha thamani yake hali iliyopelekea hadi baadhi ya wasanii kuandika barua za kujitoa katika mchakato huo

Alisema kuwa msanii anaona anajishusha thamani yake kwa kuwa na kazi bora ambazo zinafanya vyema katika tasnia ya muziki huku wadau wa muziki wakiamini msanii fulani anasifa ya kupokea tuzo hali inabadilika na kuwa tofauti na matarajio ya wadau pamoja na wasanii wenyewe

"Msanii anakubalika hususani kwa wadau hata sisi wenyewe tunaamini fulani anastahili kupata tunzo kutokana na kile anachokifanya ila hali inakuja tofauti wanapokea tunzo watu wasiostahili kabisa, hali inayosababisha wasanii kujiona anajishusha thamani yake" alisema Professor Jay

Aliongezea kuwa "Tunzo zinaonekana kama zinaupendeleo kwani wanawashirikisha wadau wa muziki ila hali inaonekana ni tofauti hivyo wanatakiwa kufanyia kazi upya mchakato huo ili kuboresha msanii anyefanya kitu bora hapa tunzo ila anayebbaisha ndiye anayenyakua tunzo hizo "

Kutokana na hali hiyo pamoja na malalamiko yaliyojitokeza katika mchakato huo aliwaomba waandaaji wa tuzo hizo kufanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha tunzo za mwaka huu zinakuwa na tija kwa wasanii pamoja na wadau ili kufikisha muziki sehemu inayostahili

Aliweka wazi kuwa tunzo ni kitu kizuri kwa nchi yoyote inayoendelea hususani tunzo kama hizo zinazoshirikisha jamii moja kwa moja kwa kupiga kura aliwataka waandaaji kuzitendea haki tunzo hizo ili zisipoteze maana halisi na kuamini kuwa mwaka huu watakuwa wameziboresha

Tunzo za muziki Killimanjaro award ni tunzo zinazofanyika kila mwaka zikiwa na lengo la kuwatunuku wasanii wa muziki kiujumla waliofanya vizuri kwa mwaka mzima

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging