Google PlusRSS FeedEmail

WADAU WAELEZEA CHANZO CHA MUZIKI KUPOTEA



WADAU mbalimbali wa muziki wa Tanzania wameleza chanzo kinachochangia wanamuziki wanaochipukia nyimbo zao kufa baada ya muda mfupi kutoka na kukaa kwenye gemu la muziki tofauti na muziki wa zamani

Wadau hao wameelezea kwamba kukosekana kwa ubunifu ndio chanzo cha baadhi ya wasanii wengi wa hapa nyumbani nyimbo zao kupotea au kutosikika ndani ya kipindi kifupi huku zikibaki zile ambazo ni za zamani kuendelea kufanya vizuri

Akizungumza na jarida hili mmoja wa wadau hao John Kitime ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Njenje alisema kuwa muziki wa hapa nyumbani haina ubunifu hali inayosababisha mashabiki wengi kupenda maneno ya muziki na si midundo ya upigaji wa vyombo vya muziki huo ambao ndio unaoleta maana ya muziki na kusababisha muziki huo uweze kupendwa kwa muda mrefu

Alisema kwa sababu muziki wa sasa unapendwa kwa sababu ya maneno yanayoimbwa sababu inayosababisha muziki upotee kwa muda mfupi kwani kuna maneno ya misimu yanayotumika katika baadhi ya nyimbo za hapa nyumbani hivyo nyimbo nyingi hupotea na maneno wanayotumia

Alisema kuwa nyimbo za zamani walikuwa wanajali upigaji wa vyombo vya muziki jinsi vyombo vilivyokuwa vinasikilizana na ndio sababu kubwa inayofanya mpaka sasa muziki wa zamani kuendelea kufanya vizuri na bado unawashabiki wengi

"Tunapenda muziki wa Kongo, na wa South Afrika si kwa sababu ya maneno kwani hata wanachokiimba hatukijui ila tunapenda nyimbo hizo kutokana na ubunifu wa vyombo na mpangilio wake ulivyotumika katika nyimbo hizo" alisema Kitime

Pamoja na hayo kwa upande wake prodjuza wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Simon 'Maneck' alikiri kuwa tatizo hilo lipo na alionekana kusikitishwa na hali hiyo

Alisema kuwa kwa sasa kuna ushindani mkubwa kwa upande wa wasanii na maprodjuza wa muziki hivyo kila mmoja akijalibu kujitengenezea mazingira ya kuendelea kuwepo kwenye 'gemu' la muziki hali ambayo wanashindwa kuboresha kazi zao kwa kuwa wabunifu

Alisema kuwa baadhi ya maprodjuza wamekuwa ni chanzo cha hali hiyo kwa sababu ya kushindwa kuwa wabunifu huku wanatengeneza nyimbo zinazofanana kitu ambacho kinachangia kupoteza radha ya muziki mapema

Alisema kuwa muziki wa zamani walikuwa wanazingatia ubunifu wa hali ya juu si tu kwa maprodjuza bali hadi kwa wasanii na ndio maana nyimbo zao mpaka leo zinaendelea kufanya vizuri



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging