MAKOMANDO WACHEZA SEBENE
Kundi la muziki wa kizazi kipya Makomando linaloundwa na wanamuziki Fred Felix na Said Christopher juzi limevuta hisia za mashabiki wa dansi baada ya kucheza kwa umakini sebene la kundi la Extra Bongo
Burudani ilifanyika katika mkesha wa pasaka ambapo Extra Bongo ilifanya shoo ya nguvu na kuwafanya mashabiki kutotulia vitini
Katika mkesha huo Makomando waliingia na staili yao ya kibega inayopendwa na mashabiki wengi huku wakitoa burudani kali za nyimbo zao mpya, na baada ya kupiga nyimbo zao kiongozi wa kundi hilo aliwaomba Extra Bongo kupiga sebene na kuanza kusakata rumba hali iliyowafanya mashabiki kuinuka na kupiga kelele za shangwe na furaha za kufurahia staili hiyo