MWANAMUZIKI JESSIE AVUA NGUO UWANJANI
Jessie J juzi alilazimika kubadili nguo zake baada ya kuingia uwanjani kuishuhudia Tottenham akiwa amevalia nguo nyekundu
Muimbaji huyo alikuwa kwenye uwanja wa White Hart Lane na baba yake, Stephen kuishuhudia Spurs ikiendeshwa puta na kulazimika kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Everton, lakini msichana huyo mwenye umri wa miaka 25 alilazimika kununua nguo zenye rangi ya klabu hiyo nyeupe kwa nia ya kuendana na mashabiki wengine na kufuta kosa alilolifanya