HARUSI YA KANYE UTATA MTUPU
Mama mzazi wa Kim Kardashian, Kris Jenner amesema kuwa kama kweli Kanye anampenda mwanaye amuoe bila ya kusikiliza maneno ya watu.
Siku za hivi karibuni Kanye ameingia kwenye utata mkubwa na waandishi wa habari hasa wapiga picha baada ya kukwaruzana nao mara mbili kutokana na kutotaka kufwatiliwa .
Kwa mujibu wa mtandao wa Raddaronline, mwanamuziki huyo amekuwa akichelea kufunga ndoa na mwanadada huyo akiamini kuwa anataka apate picha za kuuza katika mitandao halafu amuache kama alivyofanya kwa mumewe wa zamani Kris Humphries
Kris Jenner alisema kuwa kwa sasa yatasemwa mengi lakini kama wanapendana kwa dhati ahisi kama kuna baya litaweza tokea