SHAN AKANUSHA KUOLEWA MARA TANO
Mwigizaji Shan George, amesema kuwa anawashangaa watu wanaompa hongera ya kufunga ndoa, Anasema kuwa anawashangaa sana hata wale wanaovumisha kuwa amefunga ndoa mara nne hadi tano waka amefunga ndoa mara mbili tu, ambayo ya kwanza alifunga akiwa na umri wa miaka 16 ambapo hakuelewa maana ya ndoa ni nini.
Alifafanua kuwa ndoa yake ya pili alifunga akiwa mkubwa ingawa walishindwa kuelewana na mwenzake na kuamua kuachana.
Kauli ya Shan imekuja baada ya kuenea kwa uvumi kwenye mitandao mbalimbali huku kila mara zikiwekwa picha zinazomuonyesha kufunga ndoa na kutuhumiwa kupenda vijana.
Alieleza kuwa hajaolewa tena na hizo picha za harusi ni moja ya filamu yake ambayo alikuwa anacheza.