BAADA ya muimbaji kutoka nchini Marekani Chris Brown kuhukumiwa kufanya kazi mbalimbali za kijamii ikiwa pamoja na kusafisha mazingira kwa muda wa wiki mbili na siku mbili muimbaji huyo ameachia video yake rasmi ya wimbo aliomshirikisha rapper Nicki Minaj.
Video hiyo inayokwenda kwa jina la 'Love More', ni video iliyoongozwa na yeye mwenyewe , ameiachia ikiwa ni siku chache baada ya kuhukumiwa.
Chris alitoa taarifa juu ya ujio wa video yake mpya kupitia ukurasa wake wa Twitter iliyoambatana na ujumbe mfupi.
Chris Brown mwishoni mwa wiki iliyopita alihukumiwa upya kutokana na kesi inayomkabili ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna.
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Los Angeles baada ya kuonekana kuna mapungufu mengi katika kazi alizotakiwa kufanya kulingana na 'Probation' aliyokuwa nayo.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.