Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO ATISHIWA KIFO



MSANII  wa kizazi kipya miondoko  ya Hip Hop nchini Ney wa Mitego anahisi maisha yake yapo hatarini baada ya kupokea vitisho kutoka kwa watu mbalimbali.

Ingawa anaandamwa na  watu hao msanii huyo hakuwa tayari kuwataja wala kuwaweka wazi watu hao anaodai kumtishia maisha.

Msanii huyo anatamba na single yake inayojulikana kwa jina la 'Salaam Zao' ameandika taarifa hiyo ya kuandamwa na watu hao ambao hadi sasa hawajajulikana ni akina nani katika ukurasa wake wa Istagram.

Ney aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya watu wanamchukia yeye kutokana na kazi zake za muziki huku akibainisha kuwa watu hao wanatamani yeye apoteze maisha.

"Huu muziki sasa utanitoa roho sina ugomvi na mtu lakini kumbe kuna watu wananichukia kweli na wanatamani hata nife leo au wanitoe roho, mimi nafanya muziki vita yenu juu yangu namuachia mungu" aliandika katika mtandao wake wa Istagram.

Aliweka wazi kuwa yeye anaamini anafanya kazi nzuri hivyo hakuna mtu yoyote wa kumshusha wa kumrudisha nyuma, huku akisisitiza kuwa hata wakitumia imani za kishirikina hawatafanikiwa kwani yeye si wa kawaida.



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging