Google PlusRSS FeedEmail

FID Q AWATAKA WASANII WA HIP HOP KULITAWALA JUKWAA



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini miondoko ya Hip Hop, Farid Kubanda 'Fid Q' amewataka wasanii wa miondoko hiyo ya Hip Hop kujiwekea utamaduni wa kulitawala jukwaa pamoja na kuwaburudisha mashabiki pindi wawapo jukwaani.

Aliyazungumza hayo hivi karibuni katika fainali za mashindano ya Bongo Star Seach zilizofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ambapo aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wanaoimba Hip Hop kujifunza jinsi ya kulitawala jukwaa.

Alisema kuwa katika kuwaburudisha watu unahitajika kuwa mbunifu na siyo kubaki tu na aina ya uimbaji wa kusimama bila ya kujua ni jinsi gani utakavyoweza kuwaburudisha mashabiki wako waliojitokeza katika show yako.

"Wasanii wa hip hop wanatakiwa kujifunza kutoa burudani jukwaani na siyo kubaki tu haya miko juu hapana watafute mbinu zitakazowafanya mashabiki wakitoka kwenye shoo wapate cha kusimuliwa na walizike kwa kile walichokitarajia kukiona kwa msanii" alisema Fid Q.

Alisema kuwa ili kuboresha kazi yako lazima uchague na kuwa mbunifu pindi uwapo jukwaani ili utofautishe kazi inayosikika redion na ile inayoangaliwa jukwaani.

Aliongezea kuwa mshindi aliyepatika katika shindano hilo ameonesha uwezo wake mkubwa katika kulitawala jukwaa, pamoja na kwenda sambamba na mashabiki jambo ambalo ndilo linatakiwa kwa wasanii wengi wa muziki wa bongo fleva wa hapa nyumbani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging