KALA JEREMIA AISHUKIA BASATA
Star wa Hip Hop mwenye tungo adimu Bongo, Kala Jeremiah ametoa mtazamo wake kufuatia hatua ya baraza la sanaa Tanzania kuifungia ‘Ngoma’ ya Roma Mkatoliki ‘Viva Roma’.
Akizungumza suala hili, Kala amesema kama tatizo ni ushahidi wa kile alichokiimba Roma, basi ngoma zote zinapaswa kufungiwa kwa kuwa hazina uhalisia.
“Ushahidi gani unautaka? tuseme basi wale wanaoimba baby nakuona kwenye glass watoe basi ushahidi wao wanamuonaje mtu ndani ya glass, coz uimbaji ni unakuwa na fikra kwanza.
Nafikiri basata wameingilia na wanavuruga demokrasia, kwenye mziki wetu kuwanyima watu uhuru wa kuongea, walianza kwa vitisho zamani, kuzifungia kimya kimya sasa hivi ndio wameleta hii ya kuzifungia waziwazi kabisa” alisema Kala.
CREDIT: TIMESFM