Google PlusRSS FeedEmail

KINGWENDU KUACHA SANAA AKIPATA UBUNGE

Mchekeshaji Mkongwe nchini Rashid ‘Kingwendu’ Mwinshehe, amesema endapo wana Kisarawe wakimpa nafasi ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo ataacha Uchekeshaji.

Akizungumza kupitia kipindi cha Maskani cha Times FM, Kingwendu amedai hawezi kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja.

“Nikichaguliwa kuwa Mbunge nitaacha kuchekesha, kwa sababu watu wanaweza wakaona unafanya masihara yani hata kwenye kampeni zangu mie sichekeshi.

Kwa hiyo nikiingia mule ndani tu (Bungeni), nitakuwa nahudhuria vikao vya wasanii kama mgeni rasmi tu” alisema Kingwendu.

Katika ‘line’ nyingine, mgombea huyo kupitia chama cha wananchi CUF na UKAWA ameahidi kuweka nguvu za kutosha kuihudumia jamii.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging