Kwa mara ya 3 kwa mwaka huu rapper mmiliki wa Young Money Lil Wayne, anakumbana tena na mkono wa sheria kujibu mashtaka yanayomkabili.
Sahau kuuhusu mashtaka ya Private Jet na kutolipa ‘bills’, safari hii bosi huyu anashitakiwa na ‘modo’ wa kike aitwae Shanise Taylor kwa kutumia picha yake katika moja ya tisheti zake kinyume na makubaliano.
Kwa mujibu wa TMZ Shanise amesema alipiga picha hiyo mwaka 2011 na kampuni ya mavazi ya Trukfit, ila hakusaini makubaliano kuwa picha yake itumike katika tisheti ambayo amemuona nayo Wayne.
Dada huyo anaishutumu pia kampuni hiyo kwa ‘kuedit’ picha yake, na kumuonesha kana kwamba ‘amesaula’ nguo zote hata ‘nguo ya ndani’ hana.
Anasema amedhalilishwa kwa hiyo anataka nguo hizo ziondolewe sokoni, lakini pia alipwe mkwanja utakao mpooza machungu yake.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.