Wakati Tanzania ikiwa katika mbio za kuelekea katika uchaguzi mkuu mwishomi mwa Mwezi Dec,Rapper katika game ya bongo flever Roma Mkatoliki ,amewashukia vyama vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake kama Pastor na Tanzania katika kampeni zao za kisiasa bila ruhusa yake.
Roma amesema amewahi kushuhudia moja wapo ya kampeni ya kisiasa ikitumia nyimbo zake na amevionya vyama hivyo kuacha mara moja,au wamfuate kuongea nae ili waelewane kibiashara.
Roma amesema ametoa muda kwa vyama vya siasa vya upinzani vinavyotumia ngoma zake katika mikutano yao kampeni kumfuata ama kuacha kutumia,lasivyo atachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika hao,kwani wao wananufaika kwa kuwavuta mashabiki kwa kivuli cha ngoma zake..