Google PlusRSS FeedEmail

MARALIA NO MORE YAMPELEKA MWASITI NEW YORK


Mwasiti Almas anatarajia kuondoka leo kuelekea New York, Marekani kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za mafanikio ya kutokomeza ugonjwa huo duniani zitakayofanyika Novemba 8 mwaka huu.

herehe hizo ambazo zinajulikana kama 'Malaria No More' zitahudhuriwa na wadau, wafuasi na wawekezaji wa shirika hilo kwa ajili ya kuhamasisha zaidi michango ya mapambano dhidi ya malaria.

Mwasiti Almas ni mmoja kati ya wageni waalikwa na wanamuziki ambao ni wadau na wanaharakati walioalikwa kutumbuiza, pamoja na balozi wa Senegal, Youssou N'Dour.

Mwaliko wa Mwasiti ni moja ya kutambua kazi yake ya kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kwa kupita kila mikoa na vijiji vya nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu dhidi ya ugonjwa hatari wa Maralia.

Akiwa kama mchangiaji mkubwa katika masuala ya muziki aliamua kujiingiza kwa dhati katika kuhakikisha anapiga vita Malaria kwa sababu za kibinadamu. Mwasiti alitumika kama balozi mzuri wa kwanza katika kampeni ya Maralia Haikubaliki iliyofanyika hapa nchini.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging