Google PlusRSS FeedEmail

BONANZA LA MAKONGO LEADERS . JUMAMOSI

                                                 pws.JPG (240×320)
Bonanza maalumu linalowahusisha wanamichezo na wasanii waliowahi kusoma shule ya Sekondari Makongo-Dar es Salaam,linatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Leaders Klabu Kinondoni,Dar es Salaam

Bonanza litajulikana kama Makongo Day Bonanza,Mratibu wa tamasha hilo Boniface Pawasa alisema lengo lake ni kuwakutanisha pamoja wanafunzi hao na wa sasa,sambamba na kuhamasisha kuendeleza vipaji walivyonavyo na Pia zimealikwa shule mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo zikiwemo Jangwani,Tambaza,Jitegemee,Tegeta,Kipingu Sports Academy na nyinginezo

Baadhi ya wachezaji waliowahi kusoma Makongo ni pamoja na Juma Kaseja, Mussa Mgosi,Nico Nyagawa,Jerry Tegete,Haruna Moshi,Yahaya Akilimali, Justine Kandore,Aaron Nyanda,Muhaji Kampala,Mohamed Banka,Adam Matunga, Jemedari Said,Majuto Komu,Aman Simba,Ngawina Ngawina na Wilfred Kidau,pia kutakuwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali waliowahi kusoma Makongo pamoja na waliopo wakiwemo Dogo Janja,Mc Babu Ayoub,Seki,Bambo,Jose Mara,Kalala Junior na wengineo kibao

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging